|
Mkurugenzi Idara ya
Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na
waandishi wa habari hawapo (pichani) kuhusu kukamatwa kwa mmiliki wa Kampuni ya
FAKUNA ambaye anatuhumiwa kutaka kuitapeli Serikali baada ya kubainika kuwasilisha
nyaraka za kughushi ili asajili Gazeti la Lete Mambo leo jijini Dar es Salaam. Kulia
ni Kaimu Msajili wa Magazeti Patrick Kipangula na kushoto ni Afisa Habari wa
Idara ya Habari MAELEZO Lilian Lundo.
|
|
Baadhi ya waandishi
wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO aalipokuwa
akitoa taarifa juu ya kukamatwa kwa mtuhuhiwa aliyejaribu kughushi nyaraka za
Serikali ili asajili Gazeti leo jijini Dar es Salaam.
|
|
Mtuhumiwa
wa kughushi nyaraka za Serikali ili asajili Gazeti ambaye pia ni mmiliki wa
Kampuni ya FAKUNA Bw. Joseph Sheka akitolewa ndani ya Ofisi za Idara ya Habari –
MAELEZO punde baada ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO kumkabidhi
mtuhumiwa huyo mikononi mwa jeshi la Polisi kwa ajili ya hatua zaidi.
|
|
Pichani mtuhumiwa
Joseph Sheka akiongozwa na Askari Kanzu kuelekea kwenye gari la Polisi tayari
kwa kupelekwa Kituo cha Polisi Kati leo jijini Dar es Salaam. Sheka anatuhumiwa
kutaka kuitapeli Serikali kwa kuwasilisha nyaraka za kughushi katika Ofisi za
Msaji wa Magazeti ilia pate usajili wa Gazeti la Lete Mambo.
|
|
Watuhumiwa wakiwa
ndani ya Gari la Polisi mara baada ya kukamatwa na kukabidhiwa kwa jeshi la
Polisi leo jijini Dar es Salaam.Watuhumiwa hao wamefikishwa katika Kituo cha
Polisi cha Kati kwa mahojiano zaidi na hatua zingine zitafuatia.(Picha na: Frank Shija
|
Na Jacquiline Mrisho.
Idara ya Habari
(MAELEZO) imebaini nyaraka za kughushi zilizowasilishwa na Mmiliki wa Kampuni
ya FUKANI, Joseph Sheka wakati alipoziwasilisha kwa ajili ya kusajili gazeti la LETE
MAMBO.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa MAELEZO, Dkt.
Hassan Abbasi amesema kuwa mtuhumiwa huyo aliwasilisha nyaraka mbalimbali
akidai kuwa ni za Mamlaka ya Mapato (TRA) ambazo uchunguzi wa awali umebaini
kuwa mihuri na sahihi za baadhi ya maafisa wa Mamlaka hiyo zilizotumiwa ni za
kughushi.
“Ni vyema jamii
ikafahamu kuwa huu sio wakati wa kujaribu kuishi kwa njia zisizo halali, kila
mwananchi anapaswa kufuata taratibu zinatohitajika pindi anapotaka kupatiwa
huduma katika maeneo mbalimbali ya ofisi za Umma.
Dkt. Abbasi alitoa
rai kwa ofisi mbalimbali za Umma kuwa makini na nyaraka zinazowasilishwa na
wateja wao kwani zinaweza kuwa na malengo mbalimbali ya kuiingiza Serikali
katika matatizo hivyo kuitia hasara.
Mbali na hayo Dkt
abbasi alisisitiza kuwa wale wanaohisi waliwasilisha nyaraka zao na kuona
kwamba zina utata kuja kuzirekebisha na watakaobainika kuwa walighushi nyaraka hizo
sheria itafuata mkondo wake.
Kwa sasa Idara ya
Habari imemkabidhi mtuhumiwa katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini dar es
salaam kwa mahojiano zaidi.