WATUMISHI WA MUNGU NCHINI WAASWA KUWASAIDIA WENYE UHITAJI.
Nabii mkuu
mheshimiwa Dr.Geordavie akiombea bajeti mbalimbali za waumini
walizozileta kwa ajili ya kutolewa neno la unabii, siku ya jana
Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiwa anahubiri katika
hema la kukutania ngurumo ya upako kisongo jijini Arusha
Nabii mkuu akiwa anaendelea na huduma ya sikuu kuu
Nabii akiwa anamwaga upako kwa waumi waliohudhuria
Na woinde Shizza,Arusha
Watumishi wa
Mungu na waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini wametakiwa
kujijengea tabia ya kuwasaidia wenye uhitaji wakiwemo yatima ili nao
waweze kujisikia kama ni sehemu ya jamii.
Hayo
yalibainishwa jana na Nabii mkuu mheshimiwa Dr.Geordavie wakati akifanya
dua maalumu ya kupitisha bajeti ya watu walioshiriki katika sikukuu ya
kukusanya iliyofanyika katika hema la kukutania ngurumo ya upako
kisongo jijini Arusha.
Alisema kuwa ni
wajibu wa kila mtumishi kukusanya na kutoa kile alichonauwezo nacho
ili kuweza kuwasaidia watoto yatima ,wananchi wasiojiweza ili kuweza
kuwafanya nao wajisikie ni sehemu ya jamii
Alisema kuwa
mbali na watoto yatima pia aliwasihi makanisa ambayo yanajiweza kuweza
kusaidia yale ambayo ni machanga ili kuweza kuwapa nguvu ya kuweza
kuendelea kueneza injili na kumtangaza mungu kupitia makanisa yao.
Nabii mkuu Dr
Geordavie alisema kuwa kuwa lengo la sikukuu hii ya kukusanya
nikuwasaidia watoto yatima kwa kuwapa chakula kama mchele, sukari pamoja
na mafuta yakupikia ili nao wajisikie wanafuraha haswa katika kipindi
hichi cha sikukuu.
Alisema kuwa
licha ya misaada hiyo kwenda kwa watoto yatima, pia atatoa fedha kwa
watumishi wa mungu wenye makanisa madogo hapa nchini lengo likiwa ni
kuinua huduma zao na kuwasaidia katika kuendeleza huduma zao ikiwa ni
pamoja na ujenzi wa kanisa, ununuzi wa vyombo vya muziki na shughuli
nyingine za kanisa.
Sikukuu hii ya
kukusanya huadhimishwa na huduma ya Ngurumo ya Upako Duniani tarehe 26
ya kila mwaka, watu hutoa sadaka ya vitu mbalimbali ikiwemo fedha kwa
mujibu wa maelekezo ya Nabii Mkuu na kisha hugawanywa kwa vituo vya
watoto yatima huku fedha zikigawanywa kwa watumishi waliotuma maombi
ya kupata msaada wa kuendeleza huduma zao.
Mwaka jana
msaada wa zaidi ya shilingi milioni 15 ulitolewa na waumini wa kanisa la
Ngurumo ya upako na kugawanywa katika vituo mbalimbali vya watoto
yatima huku fedha zikigawiwa kwa baadhi ya makanisa madogo kwa ajili ya
kuwasaidia mambo mbalimbali.