WAKRISTO WALIVYOSHIRIKI IBADA YA MKESHA WA KRISMASI.
Askofu mstaafu wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa,
akisalimiana na muumini wa kanisa hilo Usahrika wa Azania Front, Violet
Muro baada ya kumpatia zawadi ya ibada mkesha wa Krismasi iliyofanyika
jana usiku jijini Dar es Salaam.
Kwaya ya Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Akbano ikitumbuiza katika ibada iliyofanyika katika kanisa hilo jijini Dar es Salaam.
Waumini wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano wakiwa kwenye ibada ya mkesha wa krismasi.
Vijana wa Kanisa la KKKT la Azania Front wakiigiza igizo la kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu Kristo.
Kwaya ya Vijana ya KKKT usharika wa Azania Front ikitoa burudani.
Kwaya ya vijana ya KKKT Usharika wa Azania Front ikiendelea kutoa burudani.
Watoto wakishiriki ibada katika Kanisa la KKKT la Azania Front
Askofu mstaafu wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa
akimsalimia muumini wa kanisa hilo, Violet Njau aliyekuwa ameongoza na
familia yake.
waumini wakiwa nje ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri usharika wa Azania Front baada ya ibada hiyo.
Kwaya ya Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph ikitoa burudani
Na Dotto Mwaibale
AMANI Duniani na hapa nchini hawezi kuletwa na matajiri bali italetwa na maskini wenye kumcha mungu.
Hayo yalisemwa na Askofu Mkuu wa
Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali
Pengo wakati akiongoza ibada ya mkesha wa Krismasi katika Kanisa la
Mtakatifu Joseph Dar es Salaam jana.
"Amani duniani na hapa nchini haiwezi kuletwa na matajiri bali italetwa na maskini wamchao kristo" alisema Pengo.
Alisema kila mmoja wetu mahali alipo akitekeleza wajibu wake ipasavyo atambue anakuwa anatekeleza amani.
Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania Dk. Alex Malasusa alisema Sikukuu ya Krismasi
inamaanisha ni amani na ndio maana watu mbalimbali wamekuwa wakipeana
zawadi kuashiria amani hivyo akawaomba wakristo na watu wote kuendeleza
amani nchini.
Katika ibada hiyo ya mkesha wa
Krismasi waumini walimiminika kwenye makanisa ya Anglikana la Mtakatifu
Albano, Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam la Mtakatifu Joseph
na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Azania Front huku
wakiburudishwa na nyimbo za kusifu mungu za kuzaliwa kristo.