IBADA MAALUMU YA KRISMASI, KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA LABARIKI WATOTO.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT
Lumala Mpya lililopo Sabasaba Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola,
hii leo Disemba 25, 2016 akihubiri kwenye ibada maalumu ya Krismasi
ambayo imeenda sambamba na kubariki watoto ikiwa ni ishara njema katika
siku hii ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Somo limetoka Kitabu cha Marko
Mtakatifu 10:07.
Ibada hiyo pia imekuwa njema kwani
Mhubiri wa Kimataifa, Josephine Miller kutoka Marekani amehitimisha
mahubiri na mafundisho yake ya mwisho ya zaidi ya wiki moja (Disemba
19-Disemba 25) katika Kanisa hilo la EAGT Lumala Mpya.
Mchungaji Miller amefurahishwa na huduma
katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya ambapo ametoa rai kwa waumini wote
kumtumikia Mungu. Ameonya juu ya wale wote wasiomwabudu Yesu Kristo
aliye kufa na kufufuka na badala yake wanaabudu miungu wengine kwa
mwamvuli wa dini kwa mnajiri ya kujipatia pesa. Somo limetoka Kitabu cha
Matendo ya Mitume 01:11
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakifuatilia mahubiri kutoka kwa Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola.
Miongoni mwa watoto waliobarikiwa hii leo katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, wakiwa wamebebwa na wazazi/walezi wao
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola (kulia)
pamoja na Mama Mchungaji, Mercy Kulola, wakiendelea na ibada ya
kuwabariki watoto katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya hii leo.
Baadhi ya akina mama wa Kanisa la EAGT
Lumala Mpya, wakiwa katika picha ya pamoja na Mchungaji Josephine Miller
kutoka Marekani baada ya kumaliza mahubiri na mafndisho yake hii leo.
Akina mama wa Kanisa la EAGT Lumala
Mpya, wakiwa katika picha ya pamoja na Mchungaji Josephine Miller kutoka
Marekani baada ya kumaliza mahubiri na mafndisho yake
Mchungaji Josephine Miller kutoka Marekani akimtakia baraka njema George Binagi, mmoja wa waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya.
Baadhi ya vijana wa Kanisa la EAGT
Lumala Mpya, wakiwa katika picha ya pamoja na Mchungaji Josephine Miller
kutoka Marekani baada ya kumaliza mahubiri na mafndisho yake hii leo.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka EAGT
Lumala Mpya, Happy Shamawele, akitumbuiza kwenye ibada ya Krismasi
katika kanisa hilo hii leo
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola (kushoto) pamoja na waumini wengine wakifuatilia ibada maalumu ya Krismasi hii leo
Mchungaji Josephine Miller (kushoto)
kutoka Marekani pamoja na Mama Mchungaji Mercy Kulola (kulia)
wakifuatilia ibada ya Krismasi hii leo
Happness Materego kutoka EAGT Lumala Mpya akifuatilia ibada
Waumini wa EAGT Lumala Mpya wakifuatilia ibada
Waumini wa EAGT Lumala Mpya wakifuatilia ibada ya Krismasi
Waumini wa EAGT Lumala Mpya wakifuatilia ibada ya Krismasi hii leo.
BMG na CLEO NEWS TZ inawatakia Krismasi Njema,
Sherehekea kwa Amani na Utulivu kwa kuzaliwa Emmanuel (Yesu), Mungu
pamoja nasi aliyeuokoa ulimwengu huu. Picha na Craty Cleophace wa EAGT Lumala Mpya.