NAIBU WAZIRI WA MAZINGIRA ASIKITISHWA NA UCHAFUNZI WA MAZINGIRA MTAA WA KEKO JIJINI DAR.
Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Luaga Mpina, akizungumza jana
baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Keko Magurumbasi B
Jijini Dar es salaam na kukuta uchambuzi wa mazingira kwenye mitaro
iliyopo katika eneo hilo ambapo aliiagiza Wakala wa Barabara Tanroad
kuhakikisha inajenga mitaro ya kutiririsha maji machafu katika eneo
hilo.
Na James Salvatory, BMG Dar
Ameagiza Tanroad kushirikiana na Dawasco
kujenga bomba kubwa la kutiririsha maji machafu ili kuzuia maji hayo
kutiririka ovyo mitaani
Uchafunzi wa mazingira Mtaa wa Keko Magurumbasi B Jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa Serikali
ya Mtaa wa Keko Magurumbasi B, Henny Sabu, amesema baadhi ya viwanda
vimekuwa vikitirisha maji taka bila kuzingatia kanuni za kimazingira na
kusababisha watoto wadogo kuchezea maji yenye sumu na kubabuka katika
mili yao.