WAKUSANYA USHURU WA MAEGESHO WA MAGARI JIJINI DAR WAONYWA.
Na James Salvatory, BMG Dar
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, ameyataka Makampuni yaliyopewa zabuni ya kukusanya ushuru wa maegesho ya magari Jijini Dar es salaam, hadi ifikapo mwezi januari mwakani yawe yameanza kutoa tiketi za kielektroniki (EFD's) na kwamba yatakayoshindwa kufanya hivyo yatavunjiwa mikataba yao.
Akizungumza jana na Wanahabari, Meya Mwita aliwataka mawakala wote Jijini humo kuanza kuwatoza watu ushuru kwa wa maegesho baada ya dakika 60 na kuwapa stakabadhi ya kuegesha magari ambayo ni ya kielektroniki.