UMIA Travel yazindua kampeni ya punguzo la bei kila Jumatano
Baada ya
kufanikiwa kwa kishindo kupitia kampeni yake ya ‘Black Friday’, kampuni
inayoongoza kwa huduma za hoteli mtandaoni barani Afrika imekuja na ofa
kabambe kwa wateja wake kila ifikapo siku ya Jumatano.
Kufuatia
mafanikio makubwa ya kampeni ya ‘Black Friday’ iliyovunja rekodi ya
mauzo kwa zaidi ya 30% kwa siku, Jumia Travel imerudi tena na ofa
kabambe inayokwenda kwa jina la ‘Travel Wednesday’ itakayokuwa
ikifanyika kila siku ya Jumatano kupitia kwenye tovuti yake.
Promosheni hii
ambayo pia itajulikana kama “Dream Deals” inajumuisha punguzo kubwa la
bei kwenye hoteli za hadhi ya juu ambazo zinazopendwa na watu wengi
ikiwa ni muendelezo wa kuwapatia wateja machaguo mengi zaidi ya sehemu
za kupumzika hususani kipindi hiki cha msimu wa sikukuu.
Ingawa kampeni
hii itaanza na idadi ya hoteli 5 ambazo zitakuwa zikitoa ofa kipindi cha
promosheni, siku za usoni idadi itaongezeka na kufikia hoteli 12 ambapo
ofa zitakuwa zikifanyika kila siku ya Jumatano na Ijumaa.
“Tumefanya hivi
ili kuweza kuwaridhisha wateja wetu na kuwawezesha kuwa na machaguo ya
huduma nafuu za kusafiri kupitia Jumia Travel. Kufuatia
muitikio mkubwa wa kampeni ya ‘Black Friday’ kutoka kwa wateja wetu
tumewaletea wapenda kusafiri wote ofa za aina yake tulizoingia
makubaliano na maelfu ya hoteli barani Afrika,” alibainisha Afisa
Mtendaji Mkuu wa Jumia Travel, Bw. Paul Midy.
Ofa hizi tayari
zimekwisha zinduliwa kwenye nchi kadhaa barani Afrika ambapo kampuni
hii ni kinara katika utoaji wa huduma za malazi na usafiri ambazo
wasafiri wengi wanaweza kuzimudu. Nchi hizo ni pamoja na Nigeria, Kenya,
Uganda, Tanzania, Ivory Coast, Cameroon, Senegal, Ethiopia, Ghana, na
Algeria.
Kama ilivyokuwa
kwenye kampeni ya ‘Black Friday’, ofa hizi kabambe pia zitakuwa
zikiendeshwa kwenye maeneo yote na nchi ambazo Jumia inafanya shughuli
zake.
“Zaidi ya 25%
ya huduma za hoteli zilifanyika katika maeneo ambamo Jumia inapatikana.
Hivyo basi, ni muhimu sana kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na kampuni
zilizopo nchi zingine ili kuendelea kuvutia wateja wengi zaidi, kwani
hili ndio lilikuwa dhumuni kubwa la kubadili muonekano wa kampuni hii,”
alimalizia Bw. Midy.
Naye kwa upande
wake Meneja Mkaazi wa Jumia Travel Tanzania, Bi. Fatema Dharsee
aliongezea kwa kusema kuwa, “Tunaamini kwamba kampeni ya ofa hii
itakayokuwa ikifanyika kila siku ya Jumatano imekuja wakati muafaka
ambapo watu wengi wa ndani na nje ya nchi wameshaanza au wanatarajia
kuanza mapumziko kwa ajili ya msimu wa sikukuu.
Kupitia ofa
hizi mteja anaweza kujikuta analipia gharama nafuu za malazi katika
hoteli za hadhi ya juu pasipo kutarajia, hivyo kujikuta anaokoa kiasi
kikubwa cha fedha. Ningependa kuwasihi watu kutembelea kwenye tovuti
pamoja na mitandao yetu ya kijamii ili kupata taarifa zaidi juu ya namna
ya kufaidika na ofa hii.”
Wateja na
watanzania kwa ujumla wanaweza kupata taarifa kuhusu kampeni hii kupitia
kurasa rasmi za mitandao ya kijamii na tovuti ya Jumia Travel,
majarida, ujumbe mfupi wa maneno na mingineyo.
Orodha ya
hoteli zitakazokuwa zikitoa ofa hii ya punguzo la bei kila ifikapo siku
ya Jumatano ni pamoja na Ngare Sero Mountain Lodge, Jangwani Sea Breeze
Resort, Skippers Haven, na Golden Tulip Dar es Salaam.
Kuhusu Jumia Travel
Jumia Travel
(www.travel.jumia.com) ni kampuni nambari moja unaongoza wa huduma za
hoteli kwa njia ya mtandao barani Afrika ambao humruhusu mteja kupata
bei nzuri za hoteli zaidi ya 25,000 kwa nchi za Afrika na zaidi ya
hoteli 200,000 duniani kote.
Dhumuni letu ni
kuleta kila aina ya huduma za malazi kwenye mfumo wa mtandao na
kutengeneza njia rahisi na nafuu zaidi kwa wateja kuzilipia.
Hapa Jumia
Travel, tunao mamia ya wataalamu katika masuala ya utalii ambao
huwasiliana na wateja wetu. Ofisi zetu zinapatikana katika miji na nchi
zifuatazo Lagos (Naijeria), Accra (Ghana), Dakar (Senegali), Abidjan
(Ivory Coast), Algiers (Algeria), Douala (Cameroon), Kampala (Uganda),
Dar Es Salaam (Tanzania), Nairobi (Kenya), Addis Ababa (Ethiopia), Porto
(Ureno) na Paris (Ufaransa).
Kabla ya mwezi
Juni mwaka 2016, Jumia Travel ilikuwa ikijulikana kama Jovago.
Ilianzishwa mwaka 2013 na Jumia ambayo inaendeshwa kwa kushirikiana na
MTN, Rocket Internet, Millicom, Orange na Axas.
|