MWIMBAJI MAARUFU WA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA AFUNGA PINGU ZA MAISHA.
Mbali ya kuwa Sikukuu ya Krismasi kwa
Wakristo duniani, pia jana Disemba 25,2016 ilikuwa siku ya furaha kwa
ndugu, jamaa na marafiki wa Bwana harusi Mathew Akrama Rwekila na Bibi
harusi Agnes Martine (wawili katikati), baada ya kufunga pingu za maisha
katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
Bibi harusi ni mwimbaji maarufu wa
nyimbo za injili Jijini Mwanza, akifahamika zaidi kwa jina la Agnes
Akrama, wote wakimtumikia Mungu katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini
Mwanza.
Picha na Craty Cleophace
Maharusi na wasaidizi wao, wakimsikiliza
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpywa, Dkt.Daniel Moses
Kulola, wakati wa ibada yao
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola, akisisitiza jambo wakati wa ibada ya ndoa
Bwana harusi Mathew Akrama Rwekila na Bibi harusi Agnes Martine, wakila kiapo cha ndoa.