Kulingana na Changamoto ambazo zimekuwa zikikumba Hospitali
ya Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani mara likiwemo suala la upungufu wa Shuka pamoja na Magodoro Hospitali
hiyo imepokea Msaada wa Mashuka 200 yenye thamani ya shilingi Millioni Mbili na
laki mbili kutoka kundi la Mtandao wa
kijamii WhatsApp linalojulikana kwa jina
la Jambo Tarime.
Wakikabidhi Msaada huo kwa mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorius
Luoga katika Hospitali hiyo Kundi hili
la Mtandao wa kijamii Whats App Jambo Tarime wamedai kuwa wameamua kutoa msaada
huo baada ya kuguswa na changamoto zinzokabili Hospiali John Bosco Mbusiro
ambaye ni Diwani wa kata ya Regicheri ni kiongozi wa Kundi hilo amesema kuwa
jambo Tarime ni jukwaa la Mtandoa wa kijamii ambalo limeanzishwa kwa lengo la
kujadili changamoto za Wilaya ya Tarime ikiwa ni pamoaja na kusaidia Jamii.
|