HAJI MANARA WA SIMBA AMWOMBEA MSAMAHA JERRY MURO WA YANGA TFF
Mkuu
wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Sunday
Manara amejitokeza kwa mara ya kwanza kumuombea msamaha mtani wake Jerry
Muro ili kuifufua upya hamasa na kuongeza ushindani katika ulimwengu wa
soka la Bongo.
Jerry Muro ambaye ni Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga
amefungiwa na TFF kwa muda wa mwaka mmoja kutojihusisha na soka kutokana
na matumizi mabaya ya kauli zake kupitia vyombo vya habari mwezi Julai
mwaka huu.
Manara
katika ujumbe aliouweka kwenye mtandao wake wa Instagram akiuelekeza
kwa Rais wa TFF Jamal Malinzi, amesema katika kuadhimisha sikukuu ya
Krismasi anaona ni wakati muafaka sasa kwa Rais Malinzi kutumia mamlaka
yake kumfungulia Jerry kwa kuwa amekwishatumikia takriban nusu ya
kifungo chake na kwamba soka la Bongo linamuhitaji sana kwa sasa.
"Nimekaa
nimetafakari sana,nimeamua kumuombea msamaha mtani wangu Jerry Muro
ambaye TFF mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na mpira wa miguu,
ninafanya hivi nikijua kabisa Jerry alikosea na tayari ameshatumikia
karibia nusu ya kifungo chake, ninajua kwa kufanya hivyo atakuwa
keshajifunza lugha za kutumia na pia itakuwa fundisho kwetu sisi
wasemaji na viongozi wa vilabu kwa ujumla. "Ameandika Manara
Manara pia hakusita kukumbushia jinsi ambavyo Jerry Muro amewahi kumtolea hata yeye mwenye lugha za kuudhi "
Nnafahamu
pia Jerry aliwahi kunitolea lugha zisizostahili mimi bnafsi, lakini
yale yashapita na binafasi amenihakikishia kutorudia tena, na nnaamini
viongozi na washabiki wa Simba watanielewa dhamira yangu hii njema,
ambayo inathibitisha uungwana tulio nao wanasimba".
manara
amemaliza kwa kusema kuwa soka la Tanzania linammis sana Jerry Muro na
kuomuomba Rais Malinzi kutumia mamlaka yake kumfungulia kwa kuwa Jerry
bado alikuwa hajawa na uzoefu wa kutosha katika siasa za mpira.
Kwa
upande wake Jerry Muro amefurahi na kushukuru kuona mtani wake Haji
Manara anamkumbuka na kutumia fursa hiyo kuomba msamaha kwa shirikisho
la soka Tanzania ili aendeleze hamasa ya soka aliyokuwa ameiweka nchini
yeye na Haji Manara.