KIDOKEZO CHA MAKALA: MAISHA YA WATU NA RASILIMALI WALIZOPEWA NA MWENYEZI MUNGU.
Baadhi ya akina mama wa Kijiji cha
Ikonongo wilayani Kishapu, wakitoka Kliniki, ambapo baiskeli ni chombo
kikuu cha usafiri katika wilaya hiyo.
#BMGHabari
Upendo Hotel ni moja ya hoteli kubwa zilizoko katika Kijiji cha Nyenze wilayani Kishapu.
Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Kihapu wakimuaga mwandishi wa habari hii (hayupo pichani).
Baadhi ya wakazi wa vijiji
vinavyozunguka na mgodi wa almasi katika wilaya ya kishapu mkoani
shinyanga, wameelezea kutoridhishwa na uwepo wa wawekezaji wa madini
katika wilaya hiyo kutokana na mchango wao mdogo kwenye shughuli za
kimaendeleo.
Wakizungumza na Lake Fm, wakazi hao
wamesema bado vijiji vingi wilayani kishapu vinakumbwa na changamoto
kadhaa ikiwemo ukosefu wa huduma za afya, maji, miundombinu ya umeme
pamoja na barabara, na kwamba wajibu wao kimaendeleo umekuwa mdogo
ikilinganishwa na neema ya madini iliyopo katika wilaya hiyo.
Akizungumzia wajibu wa wawekezaji
hususani wa madini katika maeneo mbalimbali nchini, Mwanasheria kutoka
Taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora ADLG, Carolina Tizeba, amesema
sheria ya madini ya Mwaka 2010, kifungu cha 10 inawataka wawekezaji
kuwajibika kwa ajili ya maendeleo ya jamii kwenye maeneo waliyowekeza.
USIKOSE KUFUATILIA MAKALA YA "MAISHA YA WATU NA RASILIMALI
WALIZOPEWA NA MWENYEZI MUNGU" HIVI KARIBUNI, KUPITIA 102.5 LAKE FM
MWANZA NA BMG HABARI.