TAASISI YA KCRI YAWAKUMBUKA WATOTO WANAOLELEWA KITUO CHA UPENDO NA WALIOLAZWA KCMC MOSHI.
Wafanyakazi
wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) wakiwa
katika picha ya pamoja na zawadi walizopeleka katika kituo cha kulelea
Watoto Yatima cha Upendo cha mjini Moshi.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro,(KCRI)
Profesa Blandina Mbaga akisalimiana na Msimamizi wa kituo cha kulelea
watoto yatima cha Upendo cha mjini Moshi Sister Yasinta walipofika kwa
ajili ya kutoa zawadi kwa watoto wa kituo hicho.
Msimamizi
wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Upendo cha mjini Moshi,Sister
Yasinta Diwi akiwaeleza historia ya kituo hicho wafanyakazi wa taasisi
ya utafiti ya magonjwa ya binadamu Kilimanjaro (KCRI).
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) Prof
Blandina Mbaga akizungumza na Mkurugenzi wa fedha Hosptali ya Rufaa ya
KCMC,Hilda Mungure (katikati) na Elizabeth Msoka.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu
Kilimanjaro (KCRI) wakiwa wamebea zawadi kwa ajili ya watoto wa kituo
cha Upendo cha mjini Moshi.
Msimamizi
wa Kituo cha Upendo cha mjini Moshi ,Sista Yasinta Diwi akiwaongoza
watoto wanaolelewa katika kituo hicho kuwaimbia wageni waliofika katika
kituo hicho kwa ajili ya kutoa zawadi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) akitoa zawadi kwa watoto wa kituo hicho.
Wafanyakazi
wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI)
wakifurahia na watoto wanaolelewa katika kituo cha Upendo cha mjini
Moshi.
Mfanyakazi
wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) Anita
akiwapa vipande vya Keki watoto wanaolelewa katika kituo cha Upendo cha
mjini Moshi.
Mtoto
Mwenye Umri wa wiki tatu anayelelewa katika kituo cha watoto cha Upendo
baada ya kupelekwa kituoni hapo kufuatia mama wa mtoto huyo kuwa na
ugonjwa wa akili.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) Prof Blandina
Mbaga akizungumza muda mchache kabla ya kuwaona watoto waliolazwa katika
Hosptali ya Rufaa ya KCMC.
Wafanyakazi
wa Taasisi ya Utafiti ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) wakitoa zawadi kwa
watoto waliolazwa katika wodi za watoto Hosptali ya Rufaa ya KCMC.
Wafanyakazi
wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI)
wakirejea mara baada ya kutoa zawadi katika kituo cha Upendo na watoto
waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.