KATIBU MKUU UVCCM TAIFA AZINDUA MAZOEZI YA KITAIFA KWA VIJANA MKOANI KAGERA.
Kaimu katibu mkuu
UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka (MNEC) wa tatu kulia akiongoza zoezi la
jogging wilaya karagwe pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na
Serikali.
Kaimu Katibu Mkuu
UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka (katikati) akiendeleza zoezi la jogging
pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Kagera Yahaya Kateme (kusho) pamoja
na viongozi na wanachama wengine.
Na Fahadin Siraji
Kaimu katibu
mkuu Uvccm Taifa, Shaka Hamdu Shaka leo amezindua rasmi kampeni ya
mazoezi ya mwili(Jogging UVCCM) yenye kauli mbiu ya "MAZOEZI KWA AFYA"
iliyozinduliwa kitaifa wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.
Shaka
ameongozana na Mwenyekiti Uvccm mkoa wa Kagera, Yahya Kateme, Mkuu wa
Wilaya Karagwe, Godfrey Ayub Mheluka pamoja na vijana na viongozi
mbalimbali Wa Chama na Serikali Wilayani humo.
Akiongea baada
ya mazoezi hayo, Shaka amewataka Makatibu wa UVCCM ngazi za wilaya
nchini kote kuzingatia maelekezo yaliyotolewa tangu tarehe 24 mwezi
Oktoba mwaka huu ya kuanzisha klabu za mazoezi (Jogging Club).
"Nitumie fursa
hii kuwapongeza sana kwa kutambua umuhimu wa mazoezi, sasa vijana lazima
wawe wakakamavu na tayari muda wote hatuwezi kuwa na taifa la vijana
goigoi wasio jiweza kama ambavyo hata makamu wa rais alivyounga mkono
katika swala hili la mazoezi". Alisema Shaka.
Amesema Jogging
ni suala muhimu kwa vijana kwani pamoja na kujenga miili yao kuwa
imara, huwafanya kuwa wamoja wenye ushirikiano wa kudumu hususani katika
mambo mbalimbali ya kijamii'.
Shaka yuko katika ziara ya siku nane mkoani Kagera ambapo atatembelea wilaya zote nane za mkoa huo.