KAMPUNI YA SIMU YA TIGO YATAMBULISHA ZANA MPYA NA KUBORESHA ZANA YA TIGO PESA.
Mkuu wa Huduma za Kidijitali wa Tigo, Tawonga Mpore (kushoto),
akizungumza Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kutambulisha zana
mpya ya simu na kuboresha zana ya Tigo Pesa kwa watumiaji wa Smartphone.
Kulia ni Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka Tigo, Suleiman Asilia.
Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka Tigo, Suleiman Asilia (kulia), akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kazini. |
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI inayoongoza kwa mtindo wa
maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imezindua zana ya kipekee, ya
kibunifu na sahihi ambayo inatoa njia rahisi ya kununua vifurushi vya
tigo, kuboresha akaunti za wateja, kuangalia salio na muhimu zaidi
kujiweka katika mkondo wa matumizi ya data.
Kampuni hiyo pia imeboresha zana
yake ya Tigo Pesa kwa kuendelea kurahisisha njia ambazo wateja wake
wanaweza kufanya miamala yao ya kifedha kwa njia ya simu.
Akielezea zana hizo kwa vyombo vya
habari katika ofisi ya Tigo Jijini Dar es Salaam leo Mkuu wa Huduma za
Kidijitali wa Tigo, Tawonga Mpore alisema, “Zana zote za Tigo na Tigo
Pesa ni ubunifu ambao unayafanya maisha kuwa rahisi na sahihi zaidi kwa
wateja wetu.
Wateja wetu wote wanaotaka kutumia
zana hizo ni kiasi tu cha kuwa na kadi ya simu iliyosajiliwa, simu ya
kisasa (smartphone) iliyo na iOS au inayoendeshwa na mifumo ya android.
Kitu wanachotakiwa kukifanya ni
kupakua zana kutoka katika jukwaa husika na kufuata maelekezo rahisi ya
kuanza kutumia zana. Hakuna haja ya kukumbuka njia ya mkato ili
kufanya muamala. Halikadhalika ni njia nzuri sana ya kudhibiti
matumizi yako husuasni katika uhifadhi wa data.”
Mpore aliongeza kuwa Tigo pia
inazundua tena zana ya Tigo Pesa iliyoboreshwa ambayo itawawezesha
watumiaji nchini kuzifikia pochi zao za Tigo Pesa katika njia sahihi na
rahisi zaidi kuliko ilivyokuwa awali. Wateja wanweza kutuma pesa
kutoka mtandao wowote, kilipia ankara (bili), kuhamishia benki,
kuongeza salio na kutoa pesa vyote hivyo kwa ktumia smartphone zao.
Akizungumzia kuboreshwa kwa zana ya
Tigo Pesa, Mkuu wa Huduma za Kifedha wa tigo Raun Swanepoel alisema,
“Watumiaji wa Smartphone nchini wanweza kuendelea kufurahia miamala yao
ya Tigo Pesa kama kawaida kwa kasi zaidi na kwa urahisi kwa kutumia
zana mpya iliyoboreshwa ya Tigo Pesa.”
Swanepoel aliongeza; “Hivi sasa
unaweza kuangalia namba za mawasiliano ulizohifadhi katika simu yako
unapochagua kutuma pesa kupitia zana ya Tigo Pesa na hali kadhalika
kuhifadhi malipo yako ya kawaida pamoja na kuhamisha fedha kutoka benki
kwa haraka hapo baadaye.”
Alisema kutambulishwa upya kwa zana
hii inayofahamika kama Tigo Pesa App mteja hatatozwa kwa data jambo
ambalo ni sawa na ilivyo kwa Tigo App wakati unapingia katika utumiaji
wa mtandao wa Tigo.
Hali kadhalika wateja wanaweza
kuzifikia kuzifikia pochi zao za tigo Pesa wakiwa sehemu yoyote duniani
kupitia mtandao wa intaneti usiotumia nyaya Wi-Fi au au data nyingine
za simu zilizounganishwa ili mradi wawe na akaunti ya Tigo Pesa
iliyosajiliwa.
“Faida nyingine ambayo imeletwa na
zana hii kwa walio na akaunti ya fedha katika simu nchini inawapa uwezo
wa wa kufikia kwa urahisi na kwa usahihi pochi moja kwa kutumia zama
kadhaa,” alihitimisha mkuu huyo wa huduma za kifedha.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)