BENKI YA KCB YAIPIGA CHEKI TAASISI YA EAST AFRICA YA JIJINI ARUSHA.
Meneja wa Benki ya KCB tawi la Arusha
TFA Hogla Laizer (kulia) akikabidhi Msaada wa hundi ya shilingi milioni
48 kwa mkurugenzi wa shirika la Ereto East Africa foundation, Godsave
Ole Megiroo. Halfa ya Makabidhiano ilifanyika katika Ofisi za Benki hiyo
zilizopo jijini Arusha
Meneja wa Benki ya KCB tawi la Arusha TFA Hogla Laizer akizungumza katika Halfa ya Makabidhiano ya msaada
wa hundi ya shilingi milioni 48 kwa shirika la Ereto East Africa
foundation.Halfa ya Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi za Benki
hiyo zilizopo jijini Arusha.kushoto ni Mkurugenzi wa shirika hilo Godsave Ole Megiroo
Na Woinde Shizza,Arusha.
Benki
ya KCB nchini Tanzania imetoa msaada wa kiasi cha fedha cha shilingi
Milioni 48 kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya kunawa mikono
vinavyojulikana kama Hand washing station katika shule za Mairowa
Intergrity na Kondoa Intergrity zilizoko chini ya taasisi ya Ereto East
Africa Foundation.
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika ofisi za benki
hiyo ,Meneja wa Benki hiyo Tawi la Arusha Hogla Laizer amesema kuwa
msaada huo ni moja kati ya mchango wa benki hiyo kwa jamii hususan
katika suala la elimu na afya hasa katika maeneo yenye changamoto kubwa
ya maji .
Meneja
huyo amesema kuwa msaada huo tayari umezisaidia shule za Kondoa
Intergrity na Mairowa Intergrity zilizoko chini ya Ereto East Africa
Foundation .
“Katika
kuchangia elimu Benki ya KCB kwa kipindi cha miaka mitatu imetoa
misaada ya thamani ya shilingi milioni 300 ili kuboresha elimu kwa kutoa
madawati na vifaa vingine vya kuboresha huduma za elimu” Alisema Hogla
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Ereto East Africa Foundation Bwana Godsave Ole Megiro
amesema kuwa msaada huo utasaidia kutatua tatizo la magonjwa ya matumbo
na kipindu pindu yanayotokana na kutokunawa mikono kwa kuanzishwa kwa
vituo hivyo vya kunawa mikono.
Godsave
amesema kuwa wameweka vituo hivyo karibu na vyoo na karibu na mabwalo
ya kunawa mikono jambo ambalo limepunguza idadi kubwa ya wanafunzi
waliokuwa wakiugua magonjwa ya matumbo.