MKUU WA WILAYA YA ILALA MKOANI DAR ES SALAAM AKABIDHI ZAWADI ZA KAPU LA SIKUKUU.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema
(katikati), akimkabidhi zawadi, Asha Soud ambaye ni mshindi la shindano
la Kapu la Sikukuu Dar es Salaam leo, lililoendeshwa na Kampuni ya
Multichoice Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Redio cha EFM. Kutoka
kulia ni msanii Haji Salum 'Mboto' Meneja Masoko wa Multichoice
Tanzania, Alpha Joseph na Mkurugenzi wa EFM, Francis Cizza.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (katikati), akimkabidhi zawadi msanii Irene Paul.
Maelekezo ya upokeaji wa zawadi hizo yakitolewa.
DC Mjema akizungumza na wanahabari baada ya kukabidhi zawadi hizo.
Washindi wa shindano hilo wakiwa katika picha ya pamoja.
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Joseph (kulia) akimkabidhi zawadi Kelvin Mhenzi
Washindi wakiondoka na zawadi zao.
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema
ametoa zawadi mbalimbali kwa washindi 24 wa shindano la Kapu la Sikuu
lililoendeshwa na Kampuni ya Multichoice Tanzania na Kituo cha Redio cha
EFM.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi
zawadi hizo Dar es Salaam leo DC Mjema aliwataka wananchi kuendelea
kufuatilia kwa karibu vipindi mbalimbali vinavyotangazwa na kituo hicho
ili waweze kujipatia zawadi kutokana na kujibu maswali yatokanyo na
vipindi hivyo na kuweza kupata zawadi kama walizopata wenzao katika
kipindi hiki cha Sikukuu.
"Napenda kuwapongezwa EFM kwa
shindano hili kwani linatoa msukumo kwa wananchi wa kusikiliza vipindi
mbalimbali vyenye manufaa" alisema Mjema.
Meneja Masoko wa Multichoice
Tanzania, Alpha Joseph akizungumza katika hafla hiyo alisema kampuni
hiyo kupitia kisambuzi chake cha DSTV imemwaga zawadi ya visambuzi vya
kisasa vipatavyo 24 pamoja na vifurushi vya mwezi mzima kwa washindi wa
shindano hilo la Kapu la Sikuu.
"Washindi hao wataweza kusherehekea
Sikukuu ya krismas na mwaka mpya kwa kuangalia chaneli zaidi ya 70 za
DStv ikiwemo mpira wa ligi ya Hispania (Laliga) na ligi ya Uingereza"
alisema Joseph
Alpha alisema Multichoice Tanzania
haijawatunuku washindi hao 24 wa kapu la Sikuu pekee bali watanzania
wote kwa ujumla kwani hivi karibuni walishusha bei za vifurushi vyao kwa
wastani wa asilimia 16, huku kifurushi maarufu cha DStv Bomba chenye
chaneli zaidi ya 70 kikipunguzwa bei hadi sh.19,975 tu.
Zawadi hizo kwa washindi hao
zilitolewa na wasanii waigiza maarufu nchini kama Muhogo Mchungu, Riyama
Ali, Haji Salum Mboto na Hashim Kambi wanaoonekana katika Tamthilia ya
Huba.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)