WAZIRI WA MICHEZO ARIDHISHWA NA UKARABATI UWANJA WA NYAMAGANA JIJINI MWANZA. KAMPUNI YA MAFUTA MOIL YAONESHA NIA YA KUWEKA MAJUKWAA.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Nape Nhauye (wa nne kulia), akiteta jambo na Afisa Habari,
ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Atley Kuni (wa tatu kushoto)
alipotembelea uwanja mkongwe wa Nyamagana Jijini Mwanza hii leo ili
kujionea zoezi la uwekaji wa nyasi bandia kwenye uwanja huo.
Waziri Nhauye ameeleza kuridhishwa na
uwekaji wa nyasi bandia kwenye uwanja huo ambapo amewashukuru wadau wote
waliofanikisha ukarabati wake wakiwemo wajasiriamali Jijini Mwanza
ambao kodi zao zimesaidia upatikanaji wa zaidi ya shilingi Milioni 190
kutoka Halmashauri ya Jiji hilo ambazo zilizojumuishwa na dola za
Kimarekani Laki Tano zilizotolewa na Shirikisho la Soka Duniani FIFA kwa
ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
Altaf Hiran Mansoor ambaye ni mdau wa
michezo Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL,
amesema kampuni hiyo iko tayari kuchangia ukarabati wa uwanja huo
ikiwemo ujenzi wa majukwaa.
Na BMG
Itakumbukwa kwamba nyasi bandia kwa
ajili ya uwanja huu zilikwama bandarini kwa muda mrefu baada ya TFF
kutakiwa kulipiwa kodi ya zaidi ya shilingi Milioni 32 hali ambayo
ilisababisha utekelezaji wake kusuasua.
Waziri Nape Nhauye amesema Serikali
itaendelea kuboresha viwanja mbalimbali nchini kuwepo na viwanja vyenye
ubora kwa ajili ya michezo.
Aidha amebainisha kwamba Chama cha
Mapinduzi kinaomkakati wa kuhakikisha kinaingia makubaliano na makampuni
mbalimbali ili kuboresha viwanja vyake ili viwe bora zaidi na kutumika
kwa ajili ya mazoezi na michezo mbalimbali ya ndani na nje ya nchini.
Altaf Hiran Mansoor ambaye ni mdau wa
michezo Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL,
amesema kampuni hiyo iko tayari kuchangia ukarabati wa uwanja huo
ikiwemo ujenzi wa majukwaa.
Wadau wa michezo Jijini Mwanza
wamefurahishwa na uwekaji nyasi kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana ambao
ulianzishwa mwaka 1945 ambapo wamesema utaongeza chachu ya ongezeko la
mechi za mpira wa miguu Jijini Mwanza pamoja na kuongeza vyanzo vya
mapato pia.
Uwanja mkongwe wa Nyamagana sasa
unang'aa kwa viwango vingine, ambapo Waziri Nape amesema anashawishika
kuandaa mechi ya kirafiki kati ya timu za Simba na Yanga zinazoundwa na
wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itakayochezewa kwenye uwanja
huo.
Itakumbukwa kwamba Mwaka 1974 timu za
Simba na Yanga zilikutana kwenye uwanja wa Nyamagana, kwenye Fainali ya
Ligi ya Taifa ya Soka ambapo Yanga iliichapa Simba bao 2-1
Mwonekano wa Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza baada ya kuwekewa nyasi bandia