390 WAPATA MAFUNZO JUU YA KUPINGA UKEKETAJI TARIME
Ili kupinga
na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa mtoto wa kike Wilayani Tarime
mkoani Mara zikiwemo Ndoa za Utotoni na ukeketaji ambao unatarajiwa kufanyika
mwaka huu Shirika la Plan
International kwa kushirikia na na Umoja wa nchi za ulaya, Jukwaa la utu wa
mtoto CDF, na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF wamejengea uwezo
viongozi wa kamati ya ulinzi na haki za mtoto ngazi ya kata na vijiji wapatao 390 kwa lengo la kuendelea kutoa Elimu
juu ya kupinga mila na desturi zilizopitwa na wakati.
MRATIBU WA MRADI WA KUPINGA NDO ZA UTOTONI , MIMBA ZA UTOTONI NA UKEKETAJI KUTOKA SHIRIKA LA PLAN INTERNATINAL SHABAN SHABAN AKISAINI KITABU CHA WAGENI KATIKA OFISI YA KATA YA MATONGO |