KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA LAFANYIKA BARAKA KWA WAUMINI WAKE.
Waumini wa Kanisa
la EAGT LUMALA MPYA Jijini Mwanza, wakipata mahubiri, maombi na
mafundisho ya mchungaji wa kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola, katika
ibada za hii leo jumapili.
Mtumishi huyu
amefanyika Baraka kwa watu wengi kwani Mungu amekuwa akimtumia vyema
kupitia mahubiri na mafundisho yake hivyo hakikisha unafika kwenye
huduma za Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini
Mwanza.
Wengi wamebarikiwa
kupitia huduma za Mchungaji Dkt.Kulola, wameponywa, wamefanikiwa katika
shughuli zao na hakika nguvu ya Kristo inazidi kuonekana ndani ya
Kanisa la EAGT Lumala Mpya.
Na BMG
Vijana waliokoka na wenye ari ya kumtumikia Mungu kwa nguvu zote ambao ni zao la kanisa la EAGT Lumala Mpya.