WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA ZIFF AZINDUA MRADI WA UONESHAJI FILAMU BURE MKOANI GEITA.
Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu
Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo, akizungumza kwenye Uzinduzi wa
Mradi wa Uoneshaji Filamu bure kwa njia ya Sinema mkoani Geita, kwa
niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Nnauye.
Uzinduzi huo ulifanyika jana katika
Ukumbi wa Desire Park Geita ambapo Taasisi ya Sanaa Na Mazingira ya
Kijani Consult Tanzania imeanzisha kampeni ya kuonesha bure Filamu
mbalimbali kwa ajili ya kufikisha elimu kwa umma ikiwemo elimu ya
Utunzaji wa Mazingira (Mabadiliko ya Tabianchi), Ufugaji wa kuku wa
kienyeji, Usalama barabarani, Madawa ya kulevya, Madhara ya ndoa za
utotoni miongoni mwa mambo mengi ya kijamii. Mradi huo umefadhiriwa na ZIFF.
Kutokana na Mwitikio wa wanatasnia ya
Filamu mkoani Geita kuonesha shauku ya kuwa na Maonesho hayo ya Filamu,
Mhe.Kombo alisema mwakani Tamasha la Kimataifa Zanzibar pia litafanyika
mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya ZIFF ni sehemu ya kusherehekea miaka 20
tangu kuanzishwa ZIFF.
Na BMG
Mhe.Kombo alisema
mwakani Tamasha la Kimataifa Zanzibar pia litafanyika mkoani Geita ikiwa
ni sehemu ya ZIFF ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa
ZIFF.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Tanzania, Bi.Joyce Fessoo, akizungumza kwa niaba ya Serikali kwenye
uzinduzi huo ambapo aliwahakikishia Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita na
nchini kwa ujumla kwamba Serikali itahakikisha inaboresha zaidi sanaa
ya filamu ikiwemo kuendelea kutoa mafunzo ya filamu kwa wanatasnia hiyo
ili filamu zinazozalishwa ziwe na ubora.
Aidha alidokeza kwamba Serikali inatoa
baraka zote kuhusiana na Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar, pia
kufanyika mkoani Geita hapo mwakani.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali
Mstaafu, Ezekiel Kyunga, akizungumza kwenye Uzinduzi wa Uoneshaji wa
Filamu mkoani Geita, ambapo alisisitiza kwamba sanaa ni ajira hivyo
wanatasnia hiyo watumie fursa mbalimbali ikiwemo mafunzo yanayotolewa na
serikali ili kuboresha zaidi kazi zao.
Katibu wa Tamasha la Kimataifa la Filamu
Zanzibar ZIFF, Robert Manondolo, akizungumza kwenye uzinduzi huo ambapo
alibainisha kwamba ZIFF imekuwa ikitoa ufadhiri kwa taasisi mbalimbali
nchini ikiwemo Taasisi ya Kijani Consult kwa lengo la kuziwezesha
kufikisha elimu kwa umma kwa njia ya kuonesha filamu bure na kufikisha
elimu iliyokusudiwa.
Katibu Tawala Wilayani Geita, Thomas
Dimme, akizungumza kwenye uzinduzi wa Tamasha la Uoneshaji wa Filamu
bure mkoani Geita ili kufikisha elimu mbalimbali ikiwemo Ufugaji na
utunzaji wa Mazingira.
Herman Matemu (aliyesimama) ambaye ni Kaimu Afisa Tawala mkoa wa Geita, akisalimia kwenye uzinduzi huo.
Kulia ni Kuka Kahindi ambaye ni Kaimu
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sanaa na Mazingira ya Kijani Consult ya mkoani
Geita, akisoma risala kuhusiana na Mradi wa Uoneshaji Filamu Bure mkoani
Geita.
Alisema mradi huo umelenga kutoa chachu
kwa wanajamii kutumia fursa mbalimbali ikiwemo ufugaji kujipatia kipato
badala ya kutegemea shughuli moja kama vile madini. Pia kuwahimiza
kujiepusha na uharibifu wa mazingira. Yote hayo pamoja na mengine
yanafikishwa kwa wananchi kwa njia ya filamu.
Mgeni Rasmi, Waziri wa Afya katika
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la
Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (kulia)
akipokea taarifa ya mradi wa uoneshaji wa filamu bure mkoani Geita
kutoka kwa Kuka Kahindi ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Sanaa na Mazingira ya Kijani Consult ya mkoani Geita (kushoto).
Mkuu wa idara ya Habari, Kijani Consult
Tanzania, Rose Mweko, akitoa salamu zake kwenye uzinduzi wa mradi wa
kuonesha filamu bure katika maeneo ya wazi mkoani Geita.
Kutoka Kushoto ni Mwakilishi wa Balozi
wa Denimark nchini Tanzania, Dotto Kahindi, Katibu Mtendaji Bodi ya
Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fessoo na Mgeni
Rasmi, Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF,
Mhe.Mahmood Thabith Kombo, wakifuatilia kwa makini zoezi la uzinduzi wa
mradi wa Kuonesha Filamu bure mkoani Geita ili kufikisha elimu kuhusu
masuala mbalimbali kwa wanajamii.
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi wa mradi wa Kuonesha Filamu bure mkoani Geita
Wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo
Maafisa Habari mkoani Geita wakifuatilia uzinduzi wa mradi wa kuonesha filamu bure mkoani Geita
Wageni mbalimbali wakifuatilia uzinduzi wa mradi wa kuonesha filamu bure mkoani Geita
Wanahabari mkoani Geita wakifuatilia uzinduzi wa mradi wa kuonesha filamu bure mkoani Geita
Wanatasnia wa Filamu mkoani Geita
Burudani za asili mkoani Geita
Burudani za asili zikiendelea
Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Geita
wakifuatilia Uzinduzi wa Mradi wa Uoneshaji wa Filamu bure mkoani humo
ili kufikisha elimu ya masuala mabalimbali ikiwemo uharibifu wa
mazingira pamoja na ufugaji kwa njia ya filamu
Mgeni Rasmi, Waziri
wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith
Kombo (mwenye kofia) pamoja na
viongozi wengine, wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto walioshiriki
shindano fupi la kucheza muziki kwenye Uzinduzi wa Mradi wa kuonesha
Filamu bure mkoani Geita.
Mgeni Rasmi Mhe.Kombo (mwenye kofia)
pamoja na viongozi wengine, wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto,
Maisala Ibrahimu anayesoma kidato cha pili shule ya Sekondari Kangalala
(ke) na Joshua Tito anayesoma darasa la kwanza shule ya msingi Kivukoni
Geita (Me) ambao walioonesha vipaji vya hali ya juu katika kucheza
muziki.
ZIFF imetoa fursa ya kuwanunulia mavazi
ya shule watoto hao huku pia wakipata fursa ya Kuhudhuria Tamasha la
Kimataifa la Filamu katika Visiwa vya Zanzibar hapo mwakani.