|
MKURUGENZI MTENDAJI WA PANAELY FOOD PRODUCTION KUTOKA JIJINI MWANZA ROSEMARY CHARLES AKIONESHA BAADHI YA BIDHAA KWA MGENI RASMI MOSES MISIWA YOMAM MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME AMBAYE PIA NI DIWANI WA KATA YA NYAMWAGA KATIKA MAONYESHO YA WIKI YA MAHUSIANO YALIYOANDALIWA NA MGODI WA ACACIA NYAMONGO SIKU TATU. |
|
AKICHEZEA NYOKA |
|
MWENYEKITI WA KIKUNDI CHA KUSINDIKA ASALI NYAMONGO MBUYA HONEY GROUP AKIONESHA MGENI RASMI JINSI GANI MZINGA WA NYUKI WA KISASA UNAVYOFANYA KAZI. |
|
PAULINA BOMA KUTOKA MUGUMU SERENGETI ARTS GROUP AKITOA MAELEZO KWA MGENI RASMI KATIKA MAONYESHO HAYO. |
|
PAULINA AKIONESHA MOJA YA BIDHAA ANAZOTENGENEZA KWA MIKONO YAKE. |
|
BAADHI YA BIDHAA ZINAZOTENGENEZWA NA SRENGETI ARTS GROUP KUTOKA MUGUMU SERENGETI MKOANI MARA |
|
MKURUGENZI WA CHACHAKE HARDWARE NICOLAUS MGAYA AKIONGEA NA MGENI RASMI KATIKA MAONYESHO |
|
WANANCHI |
|
KATIKATI NI MENEJA WA MGODI WA ACACIA NYAMONGO SAM ROESLER KULIA KWAKE NI MGENI RSMI KATIKA MAONYESHO YALIYOANDALIWA NA MGODI HUO, MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME MOSES MISIWA YOMAM WA KWANZA KUSHOTO NI SAIMON SANGA MENEJA UFANISI NA MAHUSIANO YA JAMII ACACIA. |
|
WANANCHI WAKITEMBELEA VIBANDA | |
|
MENEJA WA SIDO MKOA WA MARA FRIDA MUNGULU AKITOA UFAFANUZI KWA MGENI RASMI JUU YA VIWANDA VIDOGOVIDOGO NA FURSA ZILIZOPO KWA WAJASIRIAMALI | | | | | | |
WANANCHI
Wilayani Tarime wametakiwa kutumia fursa zinazotolewa na wafadhili mbalimbali
ukiwemo Mgodi wa Uchimbaji wa dhahabu Acacia Uliopo Nyamongo North Mara
ili kupata ujuzi na maarifa kwa ajili ya kuimarisha ujasiriamali kwa
lengo la kupata maendeleo endelevu ili kuweza kujikwamua kichumi na
kuongeza pato la Taifa.
Hayo
yamebainishwa na Meneja wa Sido mkoa wa Mara Frida Mungulu katika Wiki ya
Mahusiano iliyoandaliwa na Mgodi wa Uchimbaji wa Dhahabu Acacia North Mara nakufanyika
katika viwanja vya shule ya Sekondari Ingwe takribani Siku tatu huku
wajasirimali mbalimbali kutoka Mkoani Mara na Mwanza wakishiriki Vyema
maonyesho hayo.
Frida
alisema kuwa Wananchi wakiwemo wazawa wanazunguka Mgodi wa uchimbaji wa Dhahabu
hawana budi kutumia vyema fursa zinazotolewa kwa lengo la kuongeza kipata huku
wakijikita katika suala zima la ujasiriamali kupitia Viwanda vidogovidogo.
|
Akiongea
na CLEO NEWS TZ Beatrice Mmbaga nambaye ni mjasrimali wa kusindika Dagaa
kutoka Musoma mjini alisema kuwa kuwa akina mama ambao wamekuwa wakifanya
biashara ya ujasiriamali wametakiwa kuboresha bidhaa zao kwa kuziongezea
thamani bidhaa hizo ili kupata kipato chenye tija.
|
|
Katika
maonyesho ya nne ya biashaya yanayoandaliwa na mgodi wa Acacia Lengo lake ni
kufungua fursa kwa wakazi wanaozunguka mgodi wa Acacia ili washirikiane katika
kujifunza mbinu za kufanya biashara zao kuweza kupata soko la bidhaa zao.
Saimoni
Sanga ni meneja uzalishaji na mahusiano mgodi wa North Mara Alisema kuwa kuwa
lengo kubwa la Wiki hiyo ya mahusiano ni kufungua fursa hasa kwa wakazi
ambao wako karibu na mgodi wakiwemo wanachi kutoka vijiji vinavyzunguka Mgodi
huo.
Sanga
amezidi kuwaomba wananchi hao hawana budi kuendelea kutoa Ushirikiano
mkubwa kwa lengo la kuleta maendeleo katika jamii inayozunguka
Mgodi huo huku akisema kuwa Mgodi utaendelea kushirikiana Vyema katika
suala zima la kutatua changamoto zinazowakabiri wakazi wa Nyamongo.
Naye
Meneja wa Mgodi wa Acacia Sam Roesler alisema kuwa katika faida inayopatikana
katika mgodi huo haina budi kutekeleza miradi ya jamii ikiwemo ujenzi wa Shule
ili kuboresha Sekta ya Elimu Afya, Maji na Miundombinu ya Barabara.
“Acacia
inampango wa maendeleo Endelevu kwa ajili ya maendeleo ya jamii ya Nyamongo kwa
lengo la kutatua changamoto tunachomba ni ushirikiano mkubwa alisema” Meneja
Mgodi.
Hata hivyo
halmashauri ya wilaya ya Tarime kupitia Mwenyekiti wake Moses Misiwa Yomami
ambaye alikuwa Mgeni rasmi alisema kuwa Halmashauri yake
itaongeza kiasi cha fedha zinazotolewa kwa ajili ya wanawake na
vijana kwa ajili ya ujasiriamali itaongeza shilingi milioni 200 ikiwa ni
nyongeza ya shilingi milioni 212 ambazo tayari zimetolewa.
Pia
Mwenyekiti Huyo aliongeza kuwa ili Halmashauri yake ishirikiane vyema na mgodi
huo mgodi hauna budi kutatua mapema changamoto zinazowakabili wanachi wake huku
wale wanastahili kulipwa fidia kulipwa mara moja kwa lengo la kuondoa Migogoro
ambayo imekuwa ijitokeza.
Maonyesho ya
mahusiano yanayofanyika kwa siku tatu yanaenda kwa kauli mbiu isemayo,
Mahusiano bora kwa maendeleo endelevu.
|