WASAIDIZI WA KISHERIA WA SHIRIKA LA EfG WAUNGA JITIHADA ZA KUFANYA USAFI
Ofisa
Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shaban
Rulimbiye (kushoto), akiwaongoza kufanya usafi Soko la Temeke Sterio
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliwa ni kuunga mkono jitihada za Rais
Dk.John Magufuli katika suala zima la usafi wa mazingira.
Msaidizi wa kisheria katika soko hilo, Batuli Mkumbukwa
akifanya usafi.
Wasaidizi wa kisheria wakiwa kazini. Kutoka kushoto ni Aisha Juma kutoka Soko la Tabata Muslim, Mashimi Mbogela na Irene Daniel.
Mifagio ikipigishwa kwata ya usafi.
Ofisa Ufuatiliaji na
Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shaban Rulimbiye
(kushoto) na Charles Beatus wakifanya usafi.
Usafi ukiendelea.
Makamu Mwenyekiti wa Soko hilo, Issa
Ndilima (kulia), akishiriki kufanya usafi. Kushoto ni Kashinde Kapambale
na Aisha Juma kutoka soko la Muslim
Msaidizi wa sheria kutoka Soko la
Mchikichini Manispaa ya Ilala, Charles Beatus (kushoto), akitoa somo kwa
wafanyabiashara wa soko hilo kuhusu ukatili wa kijinsia.
Shughuli za usafi zikiendelea.
Hapa kazi tu.
Takataka zikiondolewa sokoni hapo baada ya kufanyika usafi.
Na Dotto Mwaibale
WASAIDIZI wa
kisheria wanawake kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG),
wamemuunga mkono Rais Dk. John Magufuli katika uhimizaji wa kufanya
usafi Soko la Temeke Sterio jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
katika tukio hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki sokoni hapo Ofisa
Ufuatiliaji na Tathmini wa EFG, Shaban Rulimbiye alisema wameamua
kufanya usafi wa mazingira katika masoko sita yaliyopo chini ya mradi wa
kupinga ukatili wa kijinsia masoko unaoendeshwa na shirika hilo.
"Tunamuunga
mkono rais wetu kwa jitihada zake anazozifanya za kuhimiza usafi ndio
maana wasaidizi wetu wa kisheria kutoka katika masoko hayo tupo nao hapa
Temeke kufanya usafi na baada ya hapo watatoa elimu kwa wafanyabiashara
ya kupinga ukatili huo " alisema Rulimbiye.
Alisema
ukatili wa kijinsia masokoni si kumshika maungoni mfanyabiasha na matusi
hata pale wanawake wanapofanya biashara zao kwa kuziweka chini bila ya
kuwa katika mazingira mazuri pia ni ukatili wa kijinsia.
Alisema mpango
huo wa kufanya usafi katika masoko hayo ni endelevu na kuwa kila
Jumamosi watakuwa wakifanya hivyo kumuunga mkono rais.
Rulimbiye
aliyataja masoko ambayo yapo chini ya mradi huo ambayo yatanufaika na
usafi huo wa mazingira kuwa ni Temeke Stereo, Mchikichini, Kisutu, Feri,
Gezaulole na Tabata Muslim.
Makamu
Mwenyekiti wa soko la Temeke Sterio, Issa Ndilima alilishukuru shirika
hilo kwa mpango huo wa usafi kwani umeleta hamasa kwa wafanyabiashara wa
soko hasa katika mafunzo wanayopata kupitia wasaidizi wa kisheria
kupinga ukati wa kijinsia masokoni.