Na James salvatory, BMG Dar
Serikali
imeazimia kujenga Zahanati kwa kila Kijiji na Kituo cha Afya kwa kila
Kata na kuwa na Hospitali kwa kila Halimashauri kote nchini ili
kuhakikisha kila mwananchi anapata za huduma za afya popote alipo.
Mkurugenzi wa
mafunzo na maendeleo ya wataalamu kutoka wizara ya Afya,maendeleo Jamii,
jinsia wazee na watoto Dkt. Otilia Gowelle, aliyasema hayo jana kwenye
ufunguzi wa kongamano la kitaifa la Afya la siku mbili
litakalowakutanisha wataalam wa afya takriban 700 kwa lengo la
kutathimini na kujadili na kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha Afya
inchini.
Akizungumza kwa
niaba ya waziri wa afya jinsia wazee na watoto Dkt.Gowelle amesema kuwa
kwa sasa Tanzania ina vituo 8,021 ambavyo viko katika ngazi
mbalimbali za zahanati hadi hospitali isipokuwa changamoto iliyopo ni
watumishi wa afya.
Kwa upande wake
rais wa kongamano hilo la afya (THC) Dkt. Omary Chilo, alibainisha kuwa
maudhui ya kongamano hilo ni kukutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya
afya kwa lengo la kujadili changamoto zilizopo katika sekta ya afya
pamoja na kujadili njia za kukabili changamoto hizo ili kuweza
kuboresha na kuimarisha hali ya huduma za afya inchini.
Share to:
|