Na James Salvatory, BMG Dar
Jeshi la Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es salaam, limewataka wakazi wa Jiji la dar es na
wageni Kutoka sehemu mbalimbali kuwa makini na matapeli wanaotumia mbinu
za kila aina hususani viongozi wa serikali au watu mashuhuri kujipatia
fedha kwa njia za kidanganyifu.
Kamishina wa
polisi kanda hiyo, Simon Sirro, amesema hivi karibuni kumekuwa na
malalamiko mbalimbali kutoka kwa raia wa kigeni kwamba kuna waarifu
wanaotumia vibaya jina la mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda
kuwataka watoe pesa za kigeni ikiwemo dola za Kimarekani na pesa za
Kitanzania kwa madai ya kuwasaidia wanafunzi kupata vyuo nchi za nje.
Katika hatua nyingine jeshi la polisi kanda hiyo limefanikiwa
kuwakamata watuhumiwa 220 kwa tuhuma mbalimbali za kiharifu ikiwemo
kucheza kamali, unyanganyi, kubugudhi pamoja na kununua na kuuza gongo. |