a Shaban Njia
Kampuni ya
Acacia kupitia mgodi wake wa dhahabu wa Buzwagi, imekabidhi vifaa
mbalimbali katika hospitali ya halmashauri ya Mji wa Kahama kwa lengo la
kuendelea kuboresha utendaji kazi pamoja na huduma za afya hususani
mama na mtoto.
Vifaa vilivyokabidhiwa katika hospitali hiyo vina thamani ya shilingi milioni 22.4 ambapo Meneja wa mgodi huo Asa Mwaipopo alivikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu.
Vifaa
vilivyokabidhiwa ni pamoja na mashine tatu za kutengeneza Oxgeni, viti
vitano kwa ajili ya kusukumia wagonjwa, machela mbili, mashine mbili
maalumu ya umeme ya kusafishia vifaa vya upasuaji pamoja na mashine moja
ya upasuaji. |