Na Shaban Njia
Wananchi wa
Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuchangamkia fursa za
kibiashara ambazo zitakazotokea hivi karibuni wakati wa ujenzi wa bomba
la mafuta kutoka nchini Uganda kwenda katika jiji la Tanga litakopopita
wilayani hapa.
Mkuu wa Wilaya
ya Kahama, Fadhili Nkurlu, aliyasema hayo wakati akiongea na madiwani wa
halmashauri ya Msalala katika kikao maalumu cha baraza la madiwani
kilichofanyika mwishoni mwa wiki.
Nkurlu alisema katika ujenzi wa Bomba hilo la mafuta wanategemea kuwepo kwa zaidi ya ajira 1,000 kwa wakazi wa mji wa Kahama. |