MKURUGENZI MTENDAJI WA PANAELY FOOD PRODUCTION KUTOKA JIJINI MWANZA ROSEMARY CHARLES AKIONESHA BAADHI YA BIDHAA KWA MGENI RASMI MOSES MISIWA YOMAM MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME AMBAYE PIA NI DIWANI WA KATA YA NYAMWAGA KATIKA MAONYESHO YA WIKI YA MAHUSIANO YALIYOANDALIWA NA MGODI WA ACACIA NYAMONGO SIKU TATU.



AKICHEZEA NYOKA


MWENYEKITI WA KIKUNDI CHA KUSINDIKA ASALI NYAMONGO MBUYA HONEY GROUP AKIONESHA  MGENI RASMI JINSI GANI MZINGA WA NYUKI WA KISASA UNAVYOFANYA KAZI.



PAULINA BOMA KUTOKA MUGUMU SERENGETI ARTS GROUP AKITOA MAELEZO KWA MGENI RASMI KATIKA MAONYESHO HAYO.
PAULINA AKIONESHA MOJA YA BIDHAA ANAZOTENGENEZA KWA MIKONO YAKE.


BAADHI YA BIDHAA ZINAZOTENGENEZWA NA SRENGETI ARTS GROUP KUTOKA MUGUMU SERENGETI MKOANI MARA

MKURUGENZI WA CHACHAKE HARDWARE  NICOLAUS MGAYA AKIONGEA NA MGENI RASMI KATIKA MAONYESHO
WANANCHI
KATIKATI NI MENEJA WA MGODI WA ACACIA NYAMONGO SAM ROESLER KULIA KWAKE NI MGENI RSMI KATIKA MAONYESHO YALIYOANDALIWA NA MGODI HUO, MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME MOSES MISIWA YOMAM  WA KWANZA KUSHOTO NI SAIMON SANGA MENEJA UFANISI NA MAHUSIANO YA JAMII ACACIA.
WANANCHI WAKITEMBELEA VIBANDA

 
MENEJA WA SIDO MKOA WA MARA FRIDA MUNGULU AKITOA UFAFANUZI  KWA MGENI RASMI JUU YA VIWANDA VIDOGOVIDOGO NA FURSA ZILIZOPO KWA WAJASIRIAMALI


WANANCHI Wilayani Tarime wametakiwa kutumia fursa zinazotolewa na wafadhili mbalimbali ukiwemo Mgodi wa Uchimbaji wa dhahabu Acacia Uliopo Nyamongo North Mara  ili kupata ujuzi na maarifa kwa ajili ya kuimarisha ujasiriamali kwa lengo la  kupata maendeleo endelevu ili kuweza kujikwamua kichumi na kuongeza pato la Taifa.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Sido mkoa wa Mara Frida  Mungulu katika Wiki ya Mahusiano iliyoandaliwa na Mgodi wa Uchimbaji wa Dhahabu Acacia North Mara nakufanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Ingwe  takribani Siku tatu huku wajasirimali mbalimbali kutoka Mkoani Mara na Mwanza wakishiriki Vyema maonyesho hayo.


Frida alisema kuwa Wananchi wakiwemo wazawa wanazunguka Mgodi wa uchimbaji wa Dhahabu hawana budi kutumia vyema fursa zinazotolewa kwa lengo la kuongeza kipata huku wakijikita katika suala zima la ujasiriamali kupitia Viwanda vidogovidogo.



Akiongea na CLEO NEWS TZ  Beatrice Mmbaga nambaye ni mjasrimali wa kusindika Dagaa kutoka Musoma mjini alisema kuwa kuwa akina mama ambao wamekuwa wakifanya biashara ya ujasiriamali wametakiwa kuboresha bidhaa zao kwa kuziongezea thamani bidhaa hizo ili kupata kipato chenye tija.
 


Katika maonyesho ya nne ya biashaya yanayoandaliwa na mgodi wa Acacia Lengo lake ni kufungua fursa kwa wakazi wanaozunguka mgodi wa Acacia ili washirikiane katika kujifunza mbinu za kufanya biashara zao kuweza kupata soko la bidhaa zao.

 Saimoni Sanga ni meneja uzalishaji na mahusiano mgodi wa North Mara Alisema kuwa kuwa lengo kubwa la Wiki hiyo ya mahusiano  ni kufungua fursa hasa kwa wakazi ambao wako karibu na mgodi wakiwemo wanachi kutoka vijiji vinavyzunguka Mgodi huo.

Sanga amezidi kuwaomba wananchi hao hawana budi kuendelea kutoa Ushirikiano mkubwa  kwa lengo la kuleta maendeleo katika jamii inayozunguka Mgodi  huo huku akisema kuwa Mgodi utaendelea kushirikiana Vyema katika suala zima la kutatua changamoto zinazowakabiri wakazi wa Nyamongo.

Naye Meneja wa Mgodi wa Acacia Sam Roesler alisema kuwa katika faida inayopatikana katika mgodi huo haina budi kutekeleza miradi ya jamii ikiwemo ujenzi wa Shule ili kuboresha Sekta ya Elimu Afya, Maji na Miundombinu ya Barabara.

“Acacia inampango wa maendeleo Endelevu kwa ajili ya maendeleo ya jamii ya Nyamongo kwa lengo la kutatua changamoto tunachomba ni ushirikiano mkubwa alisema” Meneja Mgodi.

Hata hivyo halmashauri ya wilaya ya Tarime kupitia Mwenyekiti wake Moses Misiwa Yomami  ambaye alikuwa Mgeni rasmi alisema kuwa Halmashauri yake   itaongeza kiasi cha fedha zinazotolewa kwa ajili ya wanawake na vijana kwa ajili ya ujasiriamali itaongeza shilingi milioni 200 ikiwa ni nyongeza ya shilingi milioni 212 ambazo tayari zimetolewa.

Pia Mwenyekiti Huyo aliongeza kuwa ili Halmashauri yake ishirikiane vyema na mgodi huo mgodi hauna budi kutatua mapema changamoto zinazowakabili wanachi wake huku wale wanastahili kulipwa fidia kulipwa mara moja kwa lengo la kuondoa Migogoro ambayo imekuwa ijitokeza.


Maonyesho ya mahusiano yanayofanyika kwa siku tatu yanaenda kwa kauli mbiu isemayo, Mahusiano bora kwa maendeleo endelevu.
Powered by Blogger.