ZAIDI
ya vijana 80 ambao wamehitimu kidato cha nne hivi karibuni mwaka huu katika
shule za sekondari mbalimbali manispaa ya Musoma mjini wameanza mafunzo ya
ujasiriamali ili yaweze kuwasaidia kufanya shughuli za uzalishaji mali kwa kipindi
cha miezi sita watakayo kuwa nyumbani wakisubiri matokeo yao.
Mafunzo
ambayo watafundishwa kwa muda usiopungua miezi miwili yamegawanywa katika
nafasi mbili tofauti ambapo nafasi ya kwanza wahitimu hao watasoma elimu ya
ujasiriamali wiki mbili darasani baada ya hapo watabuni miradi ya biashara na
kuifanya kwa vitendo(field).
Hayo
yalielezwa jana na muwezeshaji wa mafunzo hayo Boniphace Ndengo alisema mafunzo
hayo yatawasaidia vijana hao kutumia fursa ambazo ni mahitaji mbalimbali ya
jamii kwani wao ni miongoni mwa jamii hiyo kwa kuzingatia taifa linakabiliwa na
upungufu mkubwa wa wajasiriamali watu ambao ni watu wenye uwezo wa kuzalisha
firsa za ajira nchini.
’Sasa
sisi tuliona tuanze na hawa kwa sababu ni wakati muafaka yaani ukiwasubiri hadi
waende chuo kikuu ndio uwape haya mawazo unakuwa umechelewa kwa hiyo sisi
tuliona tuanze kuwafundisha wakiwa sekondari hawa walikuwa wanachama wa klabu
za jipange kufanikiwa tulizo anzisha katika shule 16 za sekondari January mwaka
huu kwa hiyo tunawaendeleza’’alisema.
Alisema
wakati huu wakiwa wanasubiri matokeo kwa muda wa miezi sita waliwaita vijana
hao na kuwapa kazi ya kufanya ambapo katika mafunzo hayo wamewataka kubuni
miradi ya biashara itakayo ingiza pato lisilopungua shilingi 150,000 kwa mwezi watafanya
kwa vitendo ambapo watasaidiwa na wajasiriamali wa aina ya biashara waliobuni
kwa kila mmoja.
‘’tuko
hapa kuwasapoti kitaaluma, na itakapo lazimu pia tutawasapoti upande wa mitaji
kwa sababu tunachama chetu cha ushirika wa akiba na mikopo imara saccoss
ambacho kinatoa mitaji kwa wajasiriamali wadogo kwa hiyo tunaweza kutoa mitaji
wa watakaohitaji ili kutekelieza mawazo ya biashara zao
walizopendekeza’’alisema.
Ndengo
alisema wanawafundisha vijana hao kanuni na mbinu ambazo zimetumiwa na watu waliofanikiwa
na kwamba wanajafribu kuwaonesha ili na wao pia waweze kufanikiwa hatua
aliyoeleza itakuwa endelevu kwa kipini cha miaka minne ambapo watawawekea
malengo ya kukuza biashara zao kwa muda wa miezi kumi na mbili.
Sabina
Juma ni miongoni mwa vijana hao alifurahia mafunzo hayo ambapo alisema anapenda
kuwa mjasiriamali elimu ambayo itamsaidia kujiajiri na kuzalisha ajira kwa
vijana wengine aliwaomba wazazi kuruhusu watoto wao kujakupata mafunzo hayo ili
taifa liondokane na changamoto ya watu wenye uwezo wa kuzalisha ajira.
Mwisho.
|