MIUNDOMBINU YA RELI JIJINI DAR ES SALAAM YAHUJUMIWA.

Na James Salvatory
Kutokana na kukithiri kwa vitendo vya hujuma na ghasia  katika miundombinu ya reli na treni vinavyofanywa na baadhi ya wananchi, uongozi wa kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetoa onyo kwa wananchi kuachana na vitendo hivyo mara moja.

Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Masanja Kadogosa, amesema baada ya Novemba 7, 2016 treni ya mizigo ya Pugu kupata ajali, baadhi ya watu walifanya fujo kwa kurusha mawe na kuharibu mabehewa saba pamoja na kujeruhi wafanyakazi wake.

Pia Kadogosa amewataka wafanyabiashara wanaofanya biashara  pembezoni mwa reli kutoa taarifa za uhalifu na kwamba wasipotoa taarifa za watu wanaofanya uharibifu wa miundombinu hiyo wataondolewa katika maeneo hayo.

Aidha hatua hiyo imefikiwa baada ya kutokea zaidi ya matukio matatu ya uharibifu wa miundombinu ya treni za TRL.

Kutokana na uharibifu huo uliojitokeza watuhumiwa 17 wanashikiliwa na jeshi la polisi na pindi upepelezi utakapokamilika watachukuliwa hatua za kisheria.

Wanaotuhumiwa na fujo pamoja na uharibifu huo ni makondakta wa dalala kwa lengo la kutisha wananchi kutoutumia usafiri wa treni" amesema.

Naibu Kamishina wa Polisi na Kamanda wa Reli, Simon Chillery amesema jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini wengine waliohusika na kitendo hicho na kuwataka wananchi kushirikiana na jeshi hilo kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Powered by Blogger.