DC LUOGA ATAEKETEZA SHAMBA LA BANGI HEKARI SABA
MKUU WA WILAYA YA TARIME LUOGA AKIFYEKA SHAMBA LA BANGI |
BANGI IKITEKETEZWA |
Mkuu
wa Wilaya ya Tarime Mkoani Mara Glorious Luoga kwa kushirikiana na kamati ya
ulinzi ya wilaya hiyo walifyeka na kuteketeza kwa moto shamba la Bangi lenye
ukubwa wa hekari saba katika mlima wa kijiji cha Weigita kata Kibasuka wilayani
humo.
Akiteketeza
mmea huo wa Bangi jana, Luoga alisema ni chanzo cha matumizi ya madawa ya
kulevya kwa vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa na kwamba imechangia ongezeko
la vichaa ambao huchanganyikiwa kwa kutumia bangi.
Luoga
alisema miezi mitatu iliyopita waliteketeza bangi katika mlima huo shamba lenye
hekari 23,ambapo jana walifyeka shamba lenye hekari saba,na kwamba zoezi hilo
ni endelevu bila kikomo ili wakulima wa zao hilo waweze kubadilika na kuanza
kulima mazao mengine ya biashara.
“Tumeendelea kuteketeza mashamba ya bangi leo hii
tumeteketeza hekari saba. Matokeo chanya yameanza kuonekana kwa kuwa eneo
tuliloteketeza leo mara ya mwisho tuliteketeza hekari 23 leo 7 maana yake
wananchi wameanza kubadilika” alisema Luoga.
Luoga
alisema wakulima wa zao hilo hulima katikati ya milima ambapo ni vigumu kubaini
mmiliki halali wa shamba,ila kwa jitihada za jeshi la polisi wamiliki hubainika
na huchukuliwa hatua mara tu baada ya kukamatwa.
“Mashamba
hayo yapo juu ya mlima tunatembea umbali wa mita 8000 kufikia shamba hilo,na
shamba sio moja,karibu milima yote iliyopo hapa wilayani,hivyo kila wiki
tunaenda kukagua mlima mmoja baada ya mwingine”alisema Luoga.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Mnanka Nyaswi alikiri mlima wa kijiji
chake kuwa na mashamba ya bangi ambapo alisema wamiliki wa mashamba hayo
hutokea kijiji jirani cha Tagota kata ya Kenyamanyori.
Nyaswi
alisema mashamba hayo ya bangi katika mlima huo yalianza tangu miaka
ya1990,ambapo uongozi wa kijiji uliopita ulikuwa ukijaribu kuzungumza na
viongozi wa kijiji hicho ili waweze kuweka katazo la kujishughulisha na kilimo
hicho,lakini ilikuwa ikishindikana.
Alisema
njia ya mkuu huyo wa wilaya ya kung’oa na kuchoma moto itasaidia kumaliza,kwa
madai kuwa endapo atakosa kuvuna kwa muda wa miaka kadhaa,mkulima huyo ataweza
kuacha kulima bangi.
Nae
mkuu wa kituo cha polisi Mjini Tarime Thomas Mapuli alisema wahusika wa mashamba
hayo watawasaka hadi watakapowakamata ili mkondo wa sheria uweze kuchukua
mkondo wake.
…Mwisho…
KUPANDA MILIMA SIYO KIDOGO |