MKUTANO wa The
African Investigative Journalism umemalizika kwa Mwaka 2016
umemalizika mapema wiki hii, kwenye chuo kikuu cha Wits hapa
Johannesburg Afrika ya Kusini na kuhudhuriwa na mamia ya
Waandishi wa Habari.
Mfuko wa Wakfu
wa Tasnia ya Habari Tanzania(TMF) ulibeba jukumu kubwa na kuitoa
Tanzania kuwa mtazamaji hadi kuwa mshiriki wa mkutano huo,
kwa kuwawezesha Waandishi wa Habari wanne kuhudhuria mkutano huo.
Nikiwa kama
mmoja kati ya washiriki wa mkutano huo kuna mengi nimejifunza
kwa muda wasiku tatu kuanzia Novemba 7 hadi 9 mwaka huu, kwa
utashi, uelewa na kutokuwa na roho ya ubinafsi, naomba ruhusa
yenu kuyaleta machache mbele yenu Waandishi wenzangu ili tuweze
kunufaika wote.
Tanzania ina
kazi nyingi zenye vigezo zikiwemo zile zilizotengenezwa chini ya
miradi ya TMF lakini Waandishi tumekuwa hatuziwakilishi kwenye majukwaa
ya kimataifa ili kazi zetu ziweze kutambulika na matokeo yake
tumekuwa tukiwaacha Waandishi wa mataifa mengine wakitamba
kwenye medali za kimataifa na kujulikana kwa kazi zao na kupata
heshima kubwa.
Nani asiyemjua
Mohamed Ali, Mwandhishi mpekuzi wa kituo cha KTN, kazi za
waandishi wetu kama zilizoibua ufisadi wa bandarini, scandal ya
Escrow na sumu ya sayanaidi kwenye mto Tegeta, ziko wapi?
Tumeshuhudia
kazi zilizofanywa na Waandishi mbali mbali zikiwakilishwa mfano Ile ya
kashifa ya rushwa kwenye michuano ya Olympic Reo de Jenairo na Ile ya
Panama paper zikitamba kweli kweli.
Napenda
kuwakumbusha kuwa, siku zote usipojikubali mwenyewe kabla mwingine
hajakukubali, naomba tulitafakari jambo hili ndugu zangu
waandishi.
Waadishi wa
Tanzania tumekuwa wazito wa kutafuta fursa za kimataifa ili
kujifunza, kuonyesha na kujijenga kiuwezo wa kitaaluma, tumekuwa
tunaacha majukwaa mengi ya kitasnia yakifanyika bila Kuwa na uwakilishi
wa Nchi.
Najua wengi
tutasema ni uwezo mdogo wa kifedha, lakini si kwelichanzo kikubwa ni
kutoona fursa mbele yenu na kutaka tuwe wakina nani kwenye
kujivunia tasnia yetuMwandishi wa upekuzi wa Kenya Mohamed Ali toka
kituo cha KTN alinena na mimi na kuniambia kuwa , anashangaa
kuona angalau watanzania kwenye mkutano huu tofauti na mikutano
mingine ya kimataifa, kwa kweli niliumia sana nikabaki naugulia
moyoni.
Nikataka kujua
mataifa mengine inakuwaje?Hapo nilibaini Kuwa, wenzetu wanafanya sana
mikakati ya kifursa na mahusiano ( lobbying na connections
development) ili kuweza kujichanganya na ulimwengu wa pamoja , wakati
sisi tunajifungia
milango kwa kuamini tunachokifanya ndicho sahihi, wakati kumbe
tunajimaliza wenyewe, nina imani kila Mwandishi mmoja mmoja
akaanza kufungua mahusiano na kuwa na jicho la mbali la kutaka
mafanikio kwenye tasnia kupitia dunia Kijiji tunaweza
kuiendeleza tasnia ya habari Tanzania,hali hii ni tofauti na
wenzetu hawapotezi hata dakika kwenye fursa.
Vyuo vya
kitaaluma na taasisi za kitaaluma vinawajibu wa kuileta tasnia kwenye
kijiji kimoja, lakini huku nyumbani wajibu wa vyombo hivyo ni mdogo sana
na havifanyi advantages analysis ya Kuwa host wa mikutano mikubwa ya
kitasnia, ni jambo hili linajidhihirisha toka kwenye mkutano huo
mkubwa kutoona uwakilishi wa taasisi za kihabari tofauti na
TMF, lakini kwa Nchi nyingine uwakilishi wa kitaasisi ni mkubwa
mno na ndio unaohamsha hamasa.
Mfano mkutano
ulioisha hapa Wits university umekibeba chuo kwa kutangaza kitivo cha
mawasiliano ya umma, washiriki wengi tumeonyesha nia ya kutaka
kusoma chuoni hapo, huo ndio mikakati ya taasisi za kitaaluma
kwenye kutafuta fursa, lakini hapo kwetu Nyumbani naona vyuo
vingi vinajitangaza kwa kutumia Vyombo vya habari tena kwa
kulipia, dunia imegeuka wenzetu wanajitangaza kwa kuleta fursa na
wakati watu wanachangamkia fursa na wao wanageuza watu hao kuwa
fursa za kitaaluma.
Faida nyingine
kwa vyuo vya kitaaluma ni kuwajenga wanafunzi wao kitaaluma,
Kuazia mkutano uanze November 7 hadi 9 wanafunzi wote wa kitivo cha
mawasiliano ya umma kuanzia degree hadi PhD walikuwa wakishiriki
matukio mbali mbali pamoja na kutafuta fursa za connections
development, je wanafunzi toka kwenye vyuo vyetu wataweza kweli
kushindana na wanafunzi kama wa Witz waliojengwa kisaikolojia na
kimahusiano ya kidunia?
Kwa kuwa sasa
tasnia ya habari inakwenda kurasimishwa kuwa taaluma ni vyema
tukajifunza toka kwa wenzetu ili nasi tuweze kupiga hatua,
natamani kuona mkutano ujao kazi za Waandishi toka Tanzania
zinatangazwa na kujulikana kimtaifa, tumechoka kuona wenzetu
wakimilki tasnia ya habari, ebu tujaribu mbona bongo movie
wameweza kila kitu ni kupanga tu na kutia nia.Kwa kupitia
fursa niliyoipata toka TMF nimejifunza mengi na nimeona bora
niandiko andiko hili fupi ili nanyi wenzangu mlisome.