MDALASINI HUSAIDIA KUPUNGUZA MAUMIVU YA HEDHI
Mdalasini ni kiungo ambacho kinapatikana kwenye magome ya miti ya mdalasini.
Hutumika kwenye vyakula vitamu. Mdalasini hutambulika kwa rangi yake ya kahawia.
FAIDA ZA MDALASINI
KUREKEBISHA UWIANO WA SUKARI MWILINI.
Iwapo mdalasini ukatumika kwenye chakula cha mtu mwenye kisukari inasaidia kurekebisha kiwango cha sukari mwilini. Pia kwa wale wenye kisukari aina ya 2 inawasaidia kuboresha uwezo wa kupokea insulini na kuweka sawa viwango vya sukari
KUPAMBANA NA VITENDO VYA KUVUJA DAMU
Kipindi unapopata majeraha mwilini seli hai za kuzuia damu kuvuja hushikana ili kuzuia damu. Kama zitakaza sana damu itaendelea kumwagika, mdalasini husaidia kuzuia kuganda kwa seli hizo
KUONGEZA UFANYAJI KAZI WA UBONGO
Harufu ya mdalasini ni nzuri na iwapo ukainusa basi husaidia kuongeza ufanyaji kazi wa ubongo
KUWEPO KWA MADINI YA CALCIUM NA FIBER HUBORESHA AFYA YA UTUMBO NA KULINDA DHIDI YA MAGONJWA YA MOYO
Mdalasini ni nyanzo za madini ya calcium, fibre na manganese. Vyote ni muhimu inasaidia kuepusha ugonjwa wa kansa ya tumbo
MAGONJWA YA HAJA KUBWA.
Madini ya fibers yalokuepo kwenye mdalasini husaidia mtu anayeharisha au kupata choo kigumu
HUPONYA MAFUA NA KIFUA
Iwapo ukatengeneza chai ya mdalasini pamoja na tangawizi basi itakupa nafuu kama una mafua au kifua
CANDIDA YEAST INFECTION( FANGASI WANAOATHIRI BAADHI YA SEHEMU ZA MWILI IKIWEMO SEHEMU ZA SIRI ZA MWANAMKE)
Mdalasini umegundulika kuwa ina uwezo wa kuzuia fangasi hao. Inavyosemekana mafuta ya mdalasini hupigana na fangasi wa candida iwapo ukachanganya chai ya mdalasini na mafuta ya magome ya mdalasini pia huongeza kinga mwilini
KUPUNGUZA UZITO
Mdalasini imegundulika inaengeza mzunguko wa damu. Kuengezeka kwa mzunguko wa damu huongeza metabolism na kusaidia mwili kupungua
TIBA YA KUCHUA
Mafuta ya mdalasini ni mazuri katika kupumzisha na kupunguza maumivu ya misuli. Tunashauriwa kupaka mafuta yake wakati wa kuchuliwa, pia unaweza kuweka matone machache kwenye maji ya kuogea kuondoa uchovu na maumivu
FANGASI WA MIGUU
Miguu inanuka au una fangasi kwenye vidole? Mafuta ya majani ya mdalasini yana nguvu ya kuponyesha tatizo hilo. Unaweza ukatumia mdalasini mzima, chai ya mdalasini au mdalasini ya unga ukachanganya na mafuta yake matone machache kisha ukaloweka miguu yako kutoa harufu mbaya au fangasi
MATATIZO YA MENO NA FIZI.
Mdalasini husaidia kuondoa bakteria bila kuharibu meno au mafizi. Mara nyingi ubani na dawa za mswaki huwa zina mafuta ya mdalasini
HEDHI
Akina mama wanaosumbuliwa na maumivu ya hedhi wanashauriwa kutumia mdalasini ambayo ndani yake kuna madini ya manganese. Imepimwa kuwa ukitumia angalau kwa siku miligramu 2 za mdalasini basi kasi ya maumivu yatapungua.
Pia unaweza kutumia ped za Neplily kutibu maumivu hayo pamoja na kusawazisha tatizo la homoni kutokuwa sawa (hormonal imbalances)
MATIBABU YA MDALASINI
(1) MATATIZO YA MOYO
Badala ya kutumia siagi na jam kwenye mkate pakaza asali na mdalasini ya unga na kula kama kifungua kinywa asubuhi. Inasadikika kuwa husaidia kuepuka kuziba mirija ya damu ya kwenye moyo, mshtuko wa moyo na kujaa mafuta kwenye mirija ya damu
(2) BARIDI YABISI AU KUPOOZA
Pakaza mafuta sehemu iliyoathirika na uchue pole pole. Na fanya chai ya asali na mdalasini na unywe kila siku kupunguza maumivu ya viungo
(3) NYWELE ZENYE KUTOKA
Changanya mafuta ya moto ya zaituni, asali kijiko 1 cha kula na mdalasini ya unga kijiko 1 cha chai pakaza kwenye nywele kaa nayo kwa dakika 15 kisha osha nywele
(4) MAAMBUKIZI YA KIBOFU Changanya mdalasini ya unga kijiko 1 cha chai, asali 1/2 kijiko cha chai na maji ya uvuguvugu na unywe. Hii husaidia kuondoa bakteria waliokuwepo kwenye mfumo wa mkojo
(5) MAUMIVU YA JINO
Pakaza mchanganyiko wa asali na mdalasini ya unga kwenue jino linalouma
(6) MAFUTA MWILINI
Tia asali na mdalasini ya unga kwenye maji ya moto au chai ya majani ya kijani(green tea) na unywe
(7) MAFUA/KIFUA
Chukua maji ya asali ya moto kiasi (asali ilochanganywa na maji) pamoja na mdalasini ya unga kidogo na unywe inasaidia kuupa mwili kinga zidi ya maradhi hasa kwa kipindi cha baridi
(8) KUVIMBIWA
Tia unga wa mdalasini kiasi kwenye kijiko cha asali na ule kabla hujala kitu hii husaidia kupunguza kiungulia na kuepuka kuvimbiwa
(9) MAISHA MAREFU
Kawaida tunashauriwa kunywa chai iliyotengenezwa pamoja na asali na mdalasini ya unga kuimarisha kinga ya mwili na kuilinda na bakteria na maradhi mengineyo
(10) CHUNUSI
Changanya asali na mdalasini kisha pakaza sehemu zenye chunusi kabla ya kulala na osha kwa maji ya uvugu vugu siku inayofuata
(11) UZITO WA KUPITILIZA
Kwa kupunguza uzito changanya asali kijiko 1 cha chai pamoja na mdalasini ya unga 1/2 kijiko cha chai pamoja na maji yaliyochemshwa kunywa kila siku asubuhi nusu saa kabla hujala chakula cha asubuhi
(12) HARUFU MBAYA MDOMONI
Sukutua maji ya uvuguvugu yaliyochanganywa na asali na mdalasini ya unga ili kufanya kinywa kisiwe na harufu mbaya
Ukiachana na asali na mdalasini kutumika kama tiba za asili pia tunashauriwa tupike vyakula vyenye kuchanganywa mdalasini na asali.
– Mafuta ya mdalasini utapata kwenye maduka ya dawa za asili