RORYA,WAJAWAZITO 858 WADAIWA KUJIFUNGULIA MAJUMBANI KWA KPINDI CHA MIEZI 3.
WAJAWAZITO 2513 wilayani
Rorya mkoani Mara wamehudhuria clinic katika vituo vya kutolea huduma ya
Afya kati ya hao 1,655 walijifungulia vituoni katka kipindi cha April-Juni/2016
huku Wazazi 858 wakiwa hawajulikani mahali walikojifungulia ambao wengi
wao wamedaiwa kujifungulia majumbani.
Diwani wa Kata ya Koryo ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu,Afya na Maji Peter Sarungi (CCM)alisema kuwa
baada ya Serikali kupitia watumishi wake kwenye vituo vya afya kutoa sharti la
kila mjamzito kuhakikisha anakwenda na mmewe clinic bila hivyo hapatiwi huduma
ya clinic imefanikisha idadi kubwa ya wanawake waliohudhuria clinic.
‘’Wajawazito waliokusudiwa ni
2925,Wajawazito waliohudhulia clinic ni 2513 na Wazazi waliojifungulia Vituo
vya kutolea huduma ya Afya ni 1655 watu 858 hawajulikani walijifungulia
wapi najua wengi wao wamejifungulia majumbani,Serikali itoe elimu kama
walivyofanya la mjamzito kwenda clinic na mme wake watafute mbinu nyingine ya
kuhakikisha kila mjamzito anajifungulia kituo cha Afya”alisema Sarungi.
Diwani wa Viti maalum Tarafa ya
luo-imbo Edina Charles (CCM) alisema kuwa kuwepo kwa umbali wa Zahanati
vijijini imeababisha wajawazito kujifungulia nyumbani au njiani kwakuwa
ushindwa kufika hili hali wakiwa na uchungu wa kujifungua na maeneo mengine
yakiwa hayana miundombinu mizuri ya barabara.
Diwani wa Kata ya Kitembe Thomas
Patric (Chadema)ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Fedha alisema kuwa kipato duni
kinakwamisha wajawazito kujifungulia hospitali kwakukoa pesa za usafiri na
gharama za hospitali ambapo pia ukwepa ili kuepuka usumbufu wa hospital.
Diwani wa kata ya Mirare Adrian
Nyawambo aliongeza” kata ina vijiji 4 lakini kituo cha Afya
kimoja, umbali wa kufika huko kilomita zaidi 5-10 ili akajifungue
hospitali anatakiwa aende Shirati au Kowak,akitoka Ingri kwenda kituo cha
afya Changuge ni mwendo wa kilomita zaidi ya 10 umbali wa huduma
unawafanya wajifungulie majumbani” alisema Nyawambo.