KIKOSI KAZI CHA WATU KUMI KITAKACHOSHAMBULIA KONGAMANO LA SAUTI YA MWANAMKE JIJINI MWANZA LEO.
Leo linafanyika Kongamano kubwa la Sauti
ya Mwanamke Jijini Mwanza kuanzia saa kumi alasiri ndani ya Gold Crest
Hotel. Kongamano limeandaliwa na kampuni ya Chocolate Princes inayoandaa
kipindi cha The Mboni Show cha Mboni Masimba.
Kuna elimu, burudani, chakula na
vinywaji kwa elfu arobaini tu hivyo usithubutu kukosa kwani kikosi cha
zaidi ya watu kumi tayari kimejipanga sawa sawa kufanya kazi yake
ipasavyo.
Tayari tiketi za kongamano hilo
litakalofanyika tarehe sita mwezi huu kwenye ukumbi wa Gold Crest Hotel
Jijini Mwanza zimeanza kuuzwa kwa shilingi elfu arobaini katika maeneo
mbalimbali ikiwemo Gold Crest Hotel, TSN Super Market Rock City Mall,
Flora Salon, Kayvies Beaty Parlour Magnum Hotel Ghana, Idda Garments,
Diamond Bar Kona ya Bwiru pamoja Bladict Classic Wear mtaa wa Uhuru
Dampo.
Na BMG Habari