EBWANAEEEEE DAR ES SALAAM TIGO FIESTA 2016 LEO IMOOOOOO!
Msanii kutoka
Nigeria, Yemi Alade (kushoto), akisalimiana na msanii Snura Mushi
alipokuwa amewasili jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Kampuni ya Simu ya
Tigo kuzungumza na wanahabari wakati akijitambulisha kwao Dar es
Salaam kuhusu uwepo wake kwenye
hitimisho la Tamasha la Fiesta litakalofanyika leo katika Viwanja vya
Leaders Klabu Jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Tamasha la Fiesta, Sebastian
Maganga (kulia), akizungumza wakati wa kuwatambulisha wasanii wa hapa
nchini na kutoka Nigeria ambao watatoa burudani leo katika viwanja vya
Leaders.
Msanii kutoka Nigeria, Yemi Alade
(kulia) , akizungumza katika mkutano wa kujitambulisha kwa waandishi wa
habari Dar es Salaam, kuhusu uwepo wake kwenye hitimisho la Tamasha la
Fiesta litakalofanyika leo viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni msanii mwenzake, Tecnomile na katikati ni msanii Snura Mushi.
Msanii Tecnomile (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Meneja Huduma wa Masoko wa Tigo, Olivier Prentout.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Picha zikipigwa na msanii Tecnomile.
***********************************
***********************************
Na Dotto Mwaibale
WASANII Yemi Alade na Tecnomile kutoka Nigeria leo watapanda jukwaani na washindi 16 washindano la Tigo Fiesta
Super Nyota katika fainali ya Tamasha la Fiesta 2016 lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika mkutano wa kujitambulisha kwa wanahabari msanii Tecnomile alisema Tanzania kwake ni kama nyumbani na Diamond na Vanesa ni washikaji zake hivyo atatoa burudani kali ili washikaji wakumbuke ujio wake.
Kwa upande wake msanii Yemi ameshukuru mapokezi makubwa yaliyofanywa dhidi yao na kuwa anaipenda Tanzania na anajisikia
yupo nyumbani na pia anakipenda Kiswahili.
Yemi alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi hasa wapenzi wa muziki kufika kwa wingi katika viwanja hivyo kupata burudani la kukata na shoka.
Tamasha la Tigo Fiesta 2016 limekuwa likiendeshwa kwa ubia baina Kampuni ya Prime Time Promotions na Tigo Tanzania
huku Tigo ikiwa ndio mdhamini mkuu.