Wanawake wakutana kutathimini mwaka mmoja wa Serikali ya Rais Magufuli.
Mwenyekiti
wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Profesa Ruth Meena (katikati) akisoma
tamko la wanawake kwa wanahabari kuelezea tathini ya mwaka mmoja wa
Serikali ya awamu ya tano mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo.
Wengine ni viongozi na wajumbe wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Profesa Ruth Meena (wa pili
kushoto) akisoma tamko la wanawake kwa wanahabari kuelezea tathini ya
mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya tano mara baada ya kufunguliwa kwa
mkutano huo. Wengine ni viongozi na wajumbe wa mkutano huo.
Aliyekuwa
mgombea nafasi ya urais wa Chama cha ACT – Wazalendo, Anna Mghwira
(kulia) ambye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho taifa akichangia mada
katika mkutano wa wanawake ulioandaliwa na Mfuko wa Wanawake Tanzania.
Baadhi
ya washiriki katika mkutano huo wakijadiliana masuala anuai. Mkutano
huo ulioshirikisha wanawake kutoka mikoa mbalimbali umefanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania, TGNP Mabibo jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa WFT, Mary Rusimbi (kushoto) akichangia mada katika mkutano huo.
Baadhi
ya wajumbe washiriki wa Mkutano wa Wanawake ulioratibiwa na Mfuko wa
Wanawake Tanzania, wakizungumza kuchangia mada mbalimbali zilizotolewa
katika mkutano huo. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Mtandao wa Jinsia Tanzania, TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya washiriki katika mkutano huo wakiserebuka na nyimbo za wanawake.
Mkutano huo ulioshirikisha wanawake kutoka mikoa mbalimbali umefanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania, TGNP Mabibo
jijini Dar es Salaam.
WANAWAKE
kupitia Mfuko wa Wanawake Tanzania wamekutaka katika mkutano na kutoa
tathimini ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na
Rais Dk. John Pombe Magufuli. Mkutano huo ulioshirikisha wanawake kutoka
mikoa mbalimbali umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtandao wa
Jinsia Tanzania, TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
katika mkutano huo, Mwenyekiti wa mfuko huo, Profesa Ruth Meena
aliipongeza Serikali ya Dk. Magufuli kwa mafanikio ilioanza kuonesha
katika ukusanyaji na usimamizi wa mapato pamoja na mapambano dhidi ya
vitendo vya rushwa huku akiiomba Serikali kutambua pia kwa vitendo
mchango wa wanawake katika ujenzi na maendeleo ya nchini.
Baadhi
ya wajumbe washiriki wa Mkutano wa Wanawake ulioratibiwa na Mfuko wa
Wanawake Tanzania, wakizungumza kuchangia mada mbalimbali zilizotolewa
katika mkutano huo. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Mtandao wa Jinsia Tanzania, TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wajumbe washiriki wa Mkutano wa Wanawake ulioratibiwa na Mfuko wa
Wanawake Tanzania, wakizungumza kuchangia mada mbalimbali zilizotolewa
katika mkutano huo. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Mtandao wa Jinsia Tanzania, TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.
Alisema
wanawake nchini watafurahia kuona Serikali ya Rais Magufuli inakisikia
kilio cha wanawake juu ya vitendo vya udhalilishwaji katika mitandao ya
kijamii, ikiwemo kuonesha uwajibikaji katika kushughulikia sheria
kandamizi ambazo bado zinaibana jamii hiyo.
"...Tunaiomba
Serikali ikemee suala la udhalilishaji wa wanawake katika mitandao ya
kijamii, Sheria ziwekwe kuwalinda wanawake. Imefanya vyema kupiga
marufuku nyimbo mbili na ngoma zinazikwenda kinyume na maadili yetu
hivyo ikemee pia pale wanawake wanapodhalilishwa," alisema Profesa
Meena.
Aidha mkutano
huo ulipongeza mfumo wa elimu bure unaotolewa sasa na Serikali kwa kuwa
unatoa fursa kwa familia maskini hasa za wanawake wajane kupata elimu
jambo ambalo awali lilikuwa changamoto kwa jamii hiyo.
Walipongeza pia
uwajibikaji unaoendelea kusimamiwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini
ya Rais Magufuli umeongeza nidhamu kazini pamoja na kuwajibika katika
utoaji huduma.
Mkutano huo
ulishirikisha wanawake wanaharakati ngazi za jamii kutoka mikoa
mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani ambapo walijadili masuala
mbalimbali ikiwemo kushirikishana changamoto kutoka maeneo yalikotoka
wajumbe wa mkutano na
kuangalia mbalengo ya baadae.