KAMPENI YA BINTI WA KITAA YAFIKA WILAYA YA TEMEKE JIJINI DAR ES SALAA.
Afisa
Mtendaji wa Wilaya ya Tandika Hija Kipeleka akizindua Rasmi kampeni ya
Binti wa kitaa katika Wilaya ya Temeke, ambapo aliwashukuru wanaoendesha
kampeni hiyo na kuahidi kushirikiana nao katika kupinga mimba na ndoa
za utotoni.
Mkurugenzi
Mtendaji wa CVIF George David Maarufu kwa jina la Ambassador Angelo
akielezea kwa kina kampeni ya Binti wa kitaa ilivyo wasaidia mabinti
wengi na kutoa ufafanuzi wa kina juu ya kampeni hiyo ambapo kwa sasa
inaendelea kuzinduliwa katika Wilaya zilizopo jijini Dar.
Mkazi
wa Mtaa wa Mvomero Tandika Bi. Rauva Maulid akieleza namna akina baba
walivyo na tabia ya kuwarubuni mabinti wenye chini ya umri wa miaka 18
na kuwababishia Mimba,na kuongeza kuwa kwa tandika watoto wengi wanapata
mimba wakiwa na miaka kuanzia miaka 12.
Mkazi
wa Mtaa wa Mvomero Said Mgeni akisisitiza kuwa wazazi wanatakiwa kuwa
jirani na watoto wao ili waweze kuwa rafiki na kuwaeleza matatizo
wanayoyapata kwa sababu kwa kufanya hivyo mabinti watakuwa huru kueleza
matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na tatizo la mimba.
Aisha mkazi wa Tandika akieleza namna vijana wanavyowarubuni na kuwasumbua ili waweze kushiriki nao katika ngono uzembe.
Mkazi
wa Mtaa wa Sheraton Tandika Fatuma akieleza namna baadhi ya mabinti
wenye umri chini ya Miaka 18 wanavyopata mimba kutokana na kurubuniwa
kufanya ngono uzembe na kuwapelekea kupata Mimba, na kuwasihi wasiwe
wepesi kudanganyika na vijana.
Binti
huyu aliyetambulika kwa jina moja tuu Mwajuma akieleza alivyo achishwa
Shule akiwa kidato cha pili kutokana na kukosa fedha za masomo hivyo
timu ya Binti wa kitaa kwa kushirikiana na Serikali ya Mtaa wa Tandika
kwa pamoja wameungana kumsomesha Binti huyo SIDO kwa kuwa anapenda kuja
kuwa mfanyabiashara.
Anaitwa
Amani Muuza Juice ya Miwa maarufu mtaa wa sokoni akielezea jinsi Mimba
za utotoni zinavyowaharibia maisha mambinti wenye umri chini ya Miaka
18, na kuwasihi wananchi wote kuipa sapoti kampeni ya Binti wa kitaa
Muwezeshaji katika uzinduzi wa kampeni ya Binti wa Kitaa Zero akitoa elimu juu ya kuzuia mimba na ndoa za utotoni
Kampeni
ya Binti wa Kitaa huwakutanisha Mabinti pamoja na watu wa rika zote,
hapa Msema chochote Steven Mfuko maarufu kwa Jina la Zero akiwa na Bibi
Zakia Seif akiwafunda mabinti wenye umri chini ya Miaka 18 kutokuwa na
papara ya kukimbilia katika ngono.
Mmoja
ya wageni waliofika katika kampeni ya Binti wa Kitaa Jesca Kitomary
alishauri kuwa wazazi wanatakiwa kuwaelimisha mabinti wao juu ya athari
za mimba za utotoni na kuolewa mapema, kwa kufanya hivyo itawasaidia
kupata mimba na kuolewa kwa muda.
Meneja
wa Kampeni ya Binti wa Kitaa Mhandisi Eliwanjeria James kutoka kikundi
cha wanawake Ma Injinia Tanzania akitoa shukurani kwa wote waliofika
katika kufanikisha uzinduzi wa Kampeni ya Binti wa kitaa katika Wilaya
ya Temeke
Mwakilishi wa Sunshine Group Fatuma akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Binti wa kitaa Temeke
Wakiendelea kufuatilia kwa makini masomo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Binti wa kitaa
Baadhi ya watu zaidi wakiwa katika pande mbalimbali wakifuatilia uzinduzi wa kampeni ya Binti wa Kitaa
Baadhi timu ya Binti wa kitaa pamoja na wakazi wa Tandika wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa