|
MKURUGENZI WA KAMPUNI YA THE LEARNERS FOUNDATION LIMITED WENDE MUBEPI AKITOE ELIMU KWA WAENDESHA PIKIPIKI KATIKA UKUMBI WA BLUE SKY HALMASHAURI YA MJI WA TARIME MKOANI MARA KUHUSU UMHIMU WA MIKOPO PAMOJA NA MATUMIZI YA KIFAA CHA GPS FASTER. |
|
AKIONGEA NA BODABODA |
|
Ili
kupunguza wimbi la uharifu hapa Nchini pamoja na wizi kwa kutumia vyombo zikiwemo pikipiki maarufu
Bodaboda kampuni ya STICLAB imezindua
kifaa maalumu cha GPS Faster ambao kinafungwa kwenye vyombo vya moto zikiwemo
pikipiki, Bajaji pamoja na Magari ili kuweza kutambua Taarifa sahihihi na
mahari chombo hicho kilipo ikiwa ni pamoja na kupunguza suala zima la uahari na
waharifu kutumia vifaa ivyo vya moto hususani pikipiki.
Akitoa Mafunzo kwa waendesha pikipiki katika ukumbi
wa Blue Sky Mjini Tarime Mkoani
Mara Mkurugenzi wa kampuni ya STICLAB Christian
Mweta kutoka Dar es salaam alisema kuwa kumekuwepo wimbi kubwa la uharifu pamoja
na wizi wa pikipiki hivyo kampuni hiyo baada ya kugundua kifaa hicho kitasaidia
kupunguza wimbi kubwa la wizi uharifa katika Maeneo mbalimbali hapa Nchini.
Christian alisema
kuwa kifaa hicho kinafanya kazi kwa kutumia mtandao pamoja ja setilaiti na pia wanaweza kupata taarifa za chombo chchote
Nchi nzima ambacho tayari kimweza
kufunguwa kifaa hicho huku mteja akiwa ameunganishwa katika simu yake pale
kifaa kinapochezewa na watu wengine anapata Taarifa kupitia ujumbe wa simu
pamoja na makao makuu
|
|
MWAKILISHI WA KAMPUNI YA THE LEARNERS FOUNDATION LIMITED (TLF)JOYCE JULIUS AKITOA SOMO KWA WAENDESHA PIKIPIKI HAO HII LEO |
|
BODABODA TARIME MJINI |
|
Wende Mubepi
ni mkurugenzi wa kampuni ya The lerner Faundation limited (TLF) kutoka Dar Es
laam alisema kuwa kampuni hiyo imefungua
fursa kwa waendesha pikipiki kwa kuingia mikataba na makampuni ya kifedha ili bodaboda hao waweze kukopeshwa na kurudisha
mikopo kwa riba nafuu ili waweze kujikwamua kiuchumi huku wakifanya Tafiti
mbalimbali na kutoa mafunzo ya ujasiliamali kwa Bodaboda hao.
Wende
alisema kuwa wanafanya kazi na kampuni hiyo
iliyozindua kifaa hicho kwani wao kama wadau chombo hicho wameweza kuingia
mkataba na benki za kifedha ili bodaboda waweze kuchukua mkopo kwa mashariti
nafuu na kuweza kufungiwa vifaa hivyo pamoja na kukata bima kwa ajili ya chombo hicho ili pale kinapopata
matatizo hawezi kurudishiwa chombo chake
Hata hivyo
mkurugezni huyo aliongeza kuwa nia ya kampuni hiyo ni kuhakikisha kila bodaboda
anamiliki chombo chake cha moto kwa lengo la kujikwamua kiuchumi na kudai kuwa
mbali na kupewa mikopo hiyo wanapewa mafunzo mbalimbali yakiwemo mafunzo ya
ujasiliamali, kujitambua ili weweze
kufanya kazi zozote pale wanapoachana na suala la bodaboda
“Tunajua bodaboda hapa nchini vyombo wanavyotumia ni
vya matajili hivyo lengo letu ni kujengea uwezo badabaoa wenyewe na kuchukua
mkopo na kurejesha polepole mpaka anapomaliza chombo hicho inakuwa mali yake
kikiwa na vifaa vyote” alisema Mkurungenzi TLF.
|
|
MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAENDESHA PIKIPIKI BODABODA MARWA MHECHI AKIONGEA NA WAENDESHA PIKIPIKI KABLA YA SEMINA KUANZA RASMI HII LEO |
|
MKURUGENZI WA KAMPUNI YA THE LEARNERS FOUNDATION LIMITED WENDE MUBEPI AKIFANYA MAHOJIANO NA MMILIKI WA CLEONEWS TZ AMBAYE PIA NI MWAKILISHI WA RFA |
|
MKURUGENZI WA STICLAB CHRISTIAN MWETA AMBAO NI WAVUNBUZI WA KIFAA
HICHO CHA GPS FASTER AKIELEZEA JINSI KINAVYOFANYA KAZI KIFAA HICHO |
|
SOMO LIKIENDELEA |
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chamacha Waendesha pikipiki
maarufu Bodabaoda wilayani taroime Tarime
Marwa Muhechi alisema kuwa kifaa hicho
kitawasaidia waendesha pikipiki ikiwa ni pamoja na kupunguza wimbi la wizi
pamoja na kusaidia jeshi la polisi katika kutambua boda boda watakao jiusisha
katika waharifu kuweka pikipiki hizo
salama muda wote.
“Sisi kama
wenyeviti wa bodaboda hapa nchhini tumekuwa tukipata changamoto mbalimbali
katika uongozi pale wizi wa pikipiki unapotokea lakini suala hili la GPS Faster
litakuwa mkombozi wetu na jeshi la polisi hivyo sasa boda nawasihi wakatumie
fursa hizi ili kuondokana na hasara wanazozipata pae pikipiki zao zinapoibiwa”
alisema Mhechi.
|
MKURUGENZI WA STICLAB CHRISTIAN MWETA AMBAO NI WAVUNBUZI WA KIFAA HICHO CHA GPS FASTER AKIELEZEA JINSI KINAVYOFANYA KAZI KIFAA HICHO |
|
MWAKILISHI WA KAMPUNI YA THE LEARNERS FOUNDATION LIMITED (TLF)JOYCE JULIUS AKITOA SOMO JUU YA UZAJAZAJI WA MIKOPO KWA BAADHI YA BODA BODA |
|
PICHA YA PAMOJA BAADA YA SEMINA |