BAYPORT TANZANIA YAADHIMISHA MIAKA 10 TANGU KUANZISHWA KWAKE NCHINI.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella
Kairuki akihutubia katika hafla ya kutimiza miaka 10 ya Taasisi ya
kifedha ya Bayport Tanzania iliyofanyika Hyatt Regency Hotel jijini Dar es Salaam juzi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mjumbe
wa Bodi ya Bayport Tanzania Mama Anna Mkapa (kushoto), na Mwenyekiti wa
bodi ya Bayport Tanzania Dkt. Ken Kwaku (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, Ali Hapi wakifurahia jambo katika hafla hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki
(kulia), Mjumbe wa Bodi ya Bayport Tanzania, Mama Anna Mkapa (katikati)
na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga, wakikata keki
katika maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Bayport Tanzania
yaliyofanyika Hyatt Regency Hotel Dar es Salaam juzi
Ni furaha tupu katika maadhimisho hayo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo.
Hafla ikiendelea.
Keki maalumu ya hafla hiyo.
Keki ikiliwa.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga (kushoto), akimlisha keki Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi.
Na Dotto Mwaibale
TAASISI ya Kifedha ya Bayport
Tanzania juzi iliadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake na kuelezea
mafanikio makubwa iliyopata ndani ya kipindi hicho.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Hyatt Regency Hotel jijini Dar es Salaam juzi, Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga alisema ndani ya miaka
10 wameweza kupiga hatua kubwa kwa kuwafikia wananchi wengi.
"Tumepiga hatua kubwa kwa kuwafikia wananchi wengi ambao wamenufaika na huduma zetu" alisema Mbaga.
Alisema kupitia taasisi hiyo wananchi wameweza kuanzisha biashara na kujenga nyumba ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto.
Mgeni rasmi wa hafla hiyo Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Angella Kairuki alisema Serikali inaipongeza taasisi hiyo kwa huduma za
mikopo inayotoa kwa wananchi hivyo kusaidia kuinua pato la taifa na mtu
mmoja mmoja.
"Changamoto kubwa iliyopo ambayo
mnapaswa kuiangalia ni riba kubwa katika mikopo yenu jaribuni
kuliangalia jambo hilo kwa karibu" alisema Kairuki.