MANISPAA YA ILEMELA YAHIMIZWA KUKABIDHI MIRADI YA UKUSANYAJI USHURU KWENYE MASOKO NA MINADA.
Viongozi mbalimbali wa
Jumuiya ya Wafanyabiashara ndogondogo katika Masoko na Minada wakiwa
kwenye picha ya pamoja na ugeni kutoka 102.5 Lake Fm Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo
Jumuiya ya
Wafanyabiashara ndogondogo katika Masoko na Minada imeuomba uongozi wa
Manispaa ya Ilemela kuipatia jukumu la kufanya usafi katika maeneo ya
hayo hatua itakayosaidia kupambana na uchafu.
Akizungumza na
Lake Fm, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoani Mwanza, Justine Sagara,
amesema hivi sasa zoezi la usafi katika maeneo ya masoko na minada
limekuwa halizingatiwi kutokana na waliopewa jukumu hilo kushindwa
kutimiza wajibu wao ipasavyo.
Amesema ipo
changamoto ya ukusanyaji wa ushuru wa usafi kutoka kwa wafanyabiashara
wa masoko na minada hivyo Jumuiya hiyo ikikabidhiwa jukumu hilo, itaweza
kufikia malengo kwa kuwa inawafahamu vyema wanachama wake na kwamba
itakuwa rahisi kuwawajibisha pale wanaposhindwa kutimiza wajibu wao.
Amesema ikiwa
Jumuiya hiyo itakabidhiwa zoezi la kukusanya ushuru wa usafi katika
masoko na minada kwenye halmashauri zote mkoani Mwanza, itawajibika
kusimamia usafi pamoja na kuwasilisha kiwango cha fedha
kinachowasilishwa na watu (vikundi) wanaokusanya ushuru huo kwa hivi
sasa.