BODI YA FILAMU NCHINI YATOA MAFUNZO KWA WASANII WA FILAMU ZAIDI YA 300 MKOANI MWANZA.
Katibu Tawala Msaidizi, kitengo cha
elimu mkoani Mwanza, Khamis Maulid, akifungua warsha ya mafunzo ya
filamu ya siku tatu mkoani Mwanza iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini
kwa ajili ya Wasanii wa Filamu mkoani Mwanza.
Na BMG
Maulid amesisitiza wasanii hao
kuhakikisha wanatengeneza filamu zenye ubora na zinazozingatia maadili
ya mtanzania na kukaguliwa kabla ya kuingia sokoni hatua ambayo
itasaidia kukuza soko la filamu mkoani Mwanza.
Pamoja na mambo mengine, warsha hiyo
imelenga kuwawawezesha kielimu wasanii wa filamu mkoani Mwanza
kutengeneza filamu zenye ubora, namna ya uanzishwa wa vikundi na kampuni
za filamu, uandishi wa miswada ya filamu,uongozi wa filamu pamoja na
taaluma ya upigaji picha.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
nchini, Joyce Fissoo, akielezea majukumu ya bodi hiyo ambayo ni pamoja
na kuhakikisha ubora wa filamu pamoja na hakimili za wasanii wa filamu
nchini.
Wasanii wa filamu mkoani Mwanza
wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo,
wakati wa warsha kwa wasanii hao hii leo.
Afisa Uendeshaji na Maso kokutoka Mfuko
wa Pensheni PPF, Khamis Mussa Khatibu, akielezea umuhimu wa wasanii wa
filamu mkoani Mwanza kujiunga na mfuko huo ili kunufaika na mafao
kutokana na kazi zao za sanaa.
PPF ni miongoni mwa wadau waliosaidia
kufanikisha warsha ya mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza
yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini.
Kutoka kushoto ni Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, Katibu Tawala Msaidizi, kitengo cha elimu mkoani Mwanza, Khamis Maulid pamoja na afisa kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF.
Mjumbe wa Bodi ya Filamu Taifa kutoka
mkoani Mwanza, Hussein Kimu (katikati) akiwa pamoja na wajumbe wengine
wa bodi hiyo pamoja na wasanii wa Filamu mkoani Mwanza.
Zaidi ya wasanii 300 wa Filamu mkoani Mwanza wakifuatilia warsha ya mafunzo ya filamu yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini.
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini,
Simon Mwakifwamba, amesema mkoani Mwanza kuna fursa nyingi kwenye soko
la filamu ikiwemo mandhari nzuri hiyo wasanii wa filamu mkoani Mwanza
watumie fursa hiyo kuboresha soko lao la filamu.
Mjumbe wa Bodi ya Filamu Taifa kutoka
mkoani Mwanza, Hussein Kimu, amesema mafunzo hayo yatawasaidia wasanii
wa Filamu mkoani Mwanza katika kuboresha filamu zao na hivyo kuinua soko
la Filamu mkoani Mwanza badala ya kutegemea soko hilo Jijini Dar es
salam pekee.
Baadhi ya wasanii wa Filamu mkoani Mwanza wakipiga picha na viongozi Filamu nchini.
Mmoja wa wasanii wa Filamu mkoani Mwanza
(kushoto) akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini,
Joyce Fissoo (katikati), kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba.
Mmoja wa wasanii wa Filamu mkoani Mwanza (kushoto) akisalimiana na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, katikati ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo
Viongozi mbalimbali, akiwemo Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba (wa kwanza kushoto), Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo (wa pili kushoto)
pamoja na Innocent Mungy kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA (wa
kwanza kulia).
Baadhi ya wasanii wa Filamu mkoani Mwanza wakipiga picha na viongozi Filamu nchini.