|
Jumamosi
Septemba 10, 2016 kuamkia jana, kinyang'anyiro kikali cha kumsaka mlimbwende wa
Kanda ya Ziwa, (OZONA MISS LAKE ZONE 2016), kimefanyika ambapo Mlimbwende,
Eluminatha Dominick (pichani) kutoka mkoani Geita ameibuka mshindi miongoni mwa
walimbwende 17 (baada ya mmoja kujitoa) waliokuwa wakiwania taji hilo.
Ushindi
wa mlimbwende huyo ulionekana kuwafurahisha mamia ya watu waliohudhuria kwenye
shindano hilo lililofanyika kwenye Viunga vya Rock City Mall Jijini Mwanza,
likiwa nimeandaliwa na kampuni ya Flora Talent Promotions chini ya Mkurugenzi
wake, Flora Lauwo na kudhaminiwa na makampuni mbalimbali ikiwemo mdhamini mkuu,
kampuni ya vipodozi ya OZONA pamoja na 102.5 Lake Fm Mwanza.
Mbunge
wa Jimbo la Geita Vijijini, Mhe.Jeseph Linzwa Kasheku Msukuma, alisema ni
furaha kubwa mkoa wa Geita kunyakua taji la Ozona Miss Lake Zone 2016 na kwamba
matarajio ni kujiandaa vyema kwa ajili ya kunyakua taji la Miss Tanzania 2016
ikiwa ni sawa sawa na matarajio aliyoyaeleza mlimbwende wa Ozona Miss Lake Zone
2016.
Na
BMG
|