Jana Septemba 10,
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za
Wilaya 11, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji 1 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa 1 ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika Halmashauri hizo.
Miongoni
mwa Wakurugenzi wa Halmashauri walioteuliwa, yumo pia mtangazaji wa kipindi cha
Clouds 360 cha Clouds Tv kinachorushwa kila siku kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.
Hudson
Stanley Kamoga ameteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.
Hii
sio mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuteua watangazaji kushika nyadhifa
mbalimbali kwani alimteua aliyekuwa Mtangazaji wa ITV, Godwin Gondwe kuwa Mkuu
wa Wilaya ya Handeni.
Wakurugenzi
wengine walioteuliwa leo ni pamoja na;-
- Mwailwa Smith
Pangani – Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
- Godfrey Sanga –
Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama
- Yusuf Daudi
Semuguruka – Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
- Bakari Kasinyo
Mohamed – Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
- Juma Ally Mnwele
– Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo
- Butamo Nuru
Ndalahwa – Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
- Waziri Mourice –
Halmashauri ya Wilaya ya Karatu
- Fatma Omar
Latu – Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo
- Godwin Emmanuel
Kunambi – Manispaa ya Dodoma
- Elias R.
Ntiruhungwa – Mji wa Tarime
- Mwantumu Dau –
Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
Frank
Bahati – Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe |