MATIKO MBUNGE CHADEMA AIMIZA KUUNDWA TIMU YA BODABODA TARIME.
Mbunge wa
jimbo la Tarime mjinikupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Esther
Matiko amezidi kuwasisitiza waendesha pikipiki maarufu boda boda kuunda timu
itakayoshiriki ligi ya Matiko Cup ambayo inatarajia kuanza huvi karibuni kwa
kushirikisha Timu zote kutoka kata Nane zilizopo katika Halmashauri ya Mji wa
Tarime kwa lengo la kuongeza na kuibua vipaji kwa wachezaji wa Soka wa aina
zote
Hayo
yamebainishwa kipindi akitia vifaa vya michezo baada ya waendesha pikipiki hao
kudai kuwa wanatarajia kuunda Timu ya waendesha pikipiki ili kuwa wanashirikia
mashindano mablimbali wilayani hapa na nje ya wilaya.
Aidha Matiko
baada ya kusikiliza kilio cha waendesha bodaboda ameweza kutoa mipira Miwili
pamoja na seti moja ya jenzi kwa ajili ya mazoezi huku akizi kusii kuanzishwa
kwa timu hiyo
Hata hivyo M
bunge aliongeza kuwa kuna baadhi ya waendesha pikipiki ni wasanii wakiwemo
waigizaji hivyo ataweza kukutana nao kwa ajili ya kufanya mazungumzo ili nini
hitaji lao kwa lengo la kuwasaidia.
Waendesha
boda boda hao walidai kuwa timu yao itakuwa mfano wa kuigwa kwani vijana wengi
wanavipaji huku wakidai lazima timu iwemimara kama timu ya stendi Shinyanga
ambayo ni ya wapiga debe.
“Kwanini
sisi bodaboda tushindwe kuunda timu na wapiga debe wameunda timu inainashiliki
ligi kuu lazima tukatimize lengo letu na vifaa tayari tumepata vya kuaznzia”
walisema.
Kwa upande
wakeMwenyekiti wa waendesha boda boda Marwa Muhechi alisema kuwa mpira ni ajila
hivyo kupitia ajila yao ya bodaboda vijana wengine wenye vipaji waweza kupata
ajila kupitia michezo hivyo ataenda kuweka mikakati ili kuwepo timu imara yenye
ushindani mkali ndani ya wilaya ya Tarime.