DC TARIME AFYEKA HEKALI 11 ZA BANGI
SHAMBA LA BANGI KABLA ALIJAFYEKWA |
Kamati
ya ulinzi na usalama wilayani Tarime mkoani mara ikiongozwa na mkuu wa wilaya
ya Tarime Glorious Luoga inaendelea na zoezi la kuteketeza madawa ya kulevya
ambayo wanachi wanaendelea na kilimo cha bangi ambapo katika kijiji cha weigita
kata ya Kibasuka Wilayani Tarime Mkoani mara Mashamba ya Bangi yenye hekali 11
yamefyekwa na kutekektezwa kwa moto huku mkuu wa wilaya huyo akisema zoezi hilo
ni endelevu kwa lengo la kukomesha zao hilo halamu.
Aidha
Luoga alisema kuwa suala la kuteketeza mashamba ya bangi ni endelevu kulingana
na wanachi na wakazi wa Tarime wanaendeleza kilimo hicho ca bangi badala ya
kulima mazao halali yanayotambuliwa na serikali
wamejikita kwenye madawa ya kulevya suala ambalo hatakubaliana nalo.
Haya
mashamba tulifyeka leo kuna mengine katika mabonde karibu na mto mara tutarudi
kwa ajili ya kuyafyeka ili kuhakikisha wanachi wetu wanalima mazao
yanayotambulika kisheria na siyo kulima bangi alisema Luoga.
Naye
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime Apoo Castro ambaye ameshiriki
zoezi hilo alisema kuwa mashamba hayo ya kilimo cha bangi wanachi wayatumie kulima mazao halali
ya chakula na biashara huku akisii wanachi kuondokana na kilimo hicho halamu.
Aidha
Mkurugenzi huyo alisema kuwa mashamba hayo
yanauwezekano wa kulima alizeti, Mbaazi mahindi pamoja na mazao mengine
hivyo kama Halmashauri wataendelea kutoa Elimu ili wanachi hao waondokane
kilimo cha na madawa ya kulevya.
BANGI IKIWA KATIKA JENGO LA MMOJA WA WAKAZI WA KATA YA KIBASUKA |
BANGI IKITEKETEZWA KWA MOTO |