BODABODA WATAKIWA KUFUATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI.
Waendesha
pikipiki maarufu boda boda wametakiwa kufuata sheria na taratibu za usalama
barabarani kwa lengo la kuepusha ajali za mara kwa mara ambazo zinapelekea
kupoteza maisha ya vijana wengi ambao ni nguvu kazi ya Taifa huku baadhi yao
wakipata vilema wa kudumu.
Swetbert
njewike ni kamishena Msaidi zi wa jeshi la Polisi Tarime Rorya kwa niaba ya
kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Tarime Rorya Andrew Satta alisema kuwa
sheria ya Nchi inatambua uwepo wa waendesha pikipiki hivyo hawana budi kufuata
sheria hizo kwa lengo la kujipatia kipato
Njewike
alisema kuwa ili kuepusha suala zima la
ajali ambazo zimekuwa zikitokea hapa nchini mara kwa mara boda boda hawana budi
kuendelea kufuata seria za usalama barabarani wakiwemo watumiaji wa vyombo vya
moto wote
“Tunajua
Serikali inatambua uwepo wa kazi zenu pia ni moja ya ujasiliama li hivyo kuna
haja kubwa ya kutumia fursa hiyo vizuri kwani baadhi ya waendesha piki wamekuwa
wakitumia vibaya fursa hiyo kwa kujiusisha katika suala za uharifu aidha kwa
kujua au bila kujua hivyo sasa munapopata taarifa za mashaka julisha jeshi la
polisi” alisema Njewike.
Ni katika
kikao cha umoja wa waendesha pikipiki Wilayani Tarime mkoani Mara kilichofanyika kwenye ukumbi wa CMG Mjini
Tarime kwa ajili ya kujadili changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na
kuendesha halambee kwa ajili ya kuendesha chama hicho yusuph Edward ni katibu
wa chama cha wandesha pikipiki wilayani Tarime akisoma risala mbele ya mgeni
rasmi wanaiomba serikali kuwapa mikopo yenye riba nafuu uku ili kujikwamua kiuchumi na kuendelea
kujiajili huku akiomba mgeni rasmi ambaye ni kamishena msaidizi wa jeshi la
Polisi Tarime Rorya Swertbert Njewike kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa
kipolisi Tarime Rorya Andrew Satta kushugulikia suala la jeshi la polisi
usalama barabara kufukuzana na waendesha pikipiki jamba ambalo linasababisha
ajali.
Esther
Matiko ni mbunge wa jimbo la Tarime mjini pia aeweza kushiriki halambe hiyo
ambapo waendesha pikipiki kupitia chama hicho ametoa shilingi millioni na
kusema kuwa ujio wa bodaboda hapa nchini umezidi kuongeza ajali hivyo amewataka
kuzingatia sheria za usalama barabarani huku akisema kuwa kupitia vikundi vyao
wataendelea kupata mikopo ya Kibenki, Halmashauri pamoja na mfuko wa jimbo
hivyo amezidi kuwasisitiza kuendeleza umoja wao.
Mwenyekiti
wa chama cha waendesha bodaboda Marwa Muhechi
akazidi kusisitiza suala zima la kusimamia sheria ambayo imetungwa kwa
mujibu wa Sheria na kuzidi kuzizingatia ambapo anazidi kusistiza kuwa gharama
imepanga kutokja shilingi Miatano na kufikia shilingi Elfu moja kwa safari zote
katika Mji wa Tarime.
Ktika halambee hiyo zimeptikana zaidi ya millioni moja ahadi jambo ambalo wmetoa shukrani waendesha boda boda hao huku wakizidi kuomba mashirika Taasisi za kifedha kuendelea kuwasaidili ili kuweza kuwa na miradi ya umoja huo kwa lengo la kuondokana na utegemezi kwani bada boda wengi uendesha pikipiki ambazo siyo zao.
MBUNGE WA JIMBO LA TARIME MJINI ESTHER MATIKO AKIONGEA NA WAENDESHA PIKIPIKI |
WAENDESHA PIKIPIKI WILAYANI TARIME MKOANI MARA. |