Tarime.
Timu ya Saongambele
Fc ya mjini Tarime imeibuka kidedea kwa kuilaza Timu ya Nyamongo Fc kichapo cha
bao 1-0 katika mashindano ya kupinga ukatili wa kijinnsia ikiwemo ndo za
utotoni, ukeketaji n maimb za utotoni.
Katioka
michuano hiyo y finali bao la kwnza limefungwa na Ben Maranja mnamo dk ya 55
kipindi cha pili n kudumu mpka dk 90 za mutanangehizo zinamalizika hu ku
nymongo Fc wakikamia vikali Songambele ili kurudisha bao hilo suala ambalo
halikuzaa mautunda.
Aidha
mashindano hayo yamefadhiliwa na Plan International kwa kushirikia na na Umoja
wa nchi za ulaya, Jukwaa la utu wa mtoto CDF, na Shirikisho la mpira wa miguu
Tanzania TFF n kutimua vumbi katika
viwanja mbalimbali wilayani hapa kupitia mpira wa miguu kwa wasichan kwa lengo la
kufikisha ujumbe kwa jamii lengo ni kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia
ukiwemo ukeketaji na ndoa za utotni wilayani Tarime Mkoani Mara ambapo
mashindano hayo yametia nanga jana katika viwanja vya serengeti maarufu shamba
la bibi Mjini Tarime huku Tarime QUEENS Wakiilaza Sirari Queens kichapo cha bao
3-1.
Timu hizo
zilikamiana mpaka dk zote za mchezo zinmalizika bila kufungna ndipo waliamua
kutandika mikwaju ya penaliti huku Tarime Queens wakitandika Sirari Queens
kichapo cha bao 3-1
Neema mzuri
kwao ni kapteni wa Tarime Queens alisema kuwa wadaua wa soka hawana budi
kuwaunga mkono ili kutimiza ndoto huku akisema kuwa ndoto za baadhi ya
wachezaji hao ni kuchezea timu ya Taifa ya wanawake Twiga stars.
“Sisi timu
yetu tunandoto za kufika mbali hadi kuchezea timu ya taifa ya wanawake” alisema
Mzuri kwao.
Shabani
shabani ni mratibu wa michezo hiyo kutoka shirika la plan Internatinal alisem akuwa ,mashindano hayo yamefanyika
vyema huku Timu mbalimbali zikichuana vikali na mwisho timu ya SongambeleFc na Nyamongo Fc zikabahatika
kuingia fainali.
Aidha
Shabani alisema kuwa kupitia mashindano hayo jamii inapata uju,be wenye lengo
la kukemea vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike.
“Haya
mashindano tunashirikisha mabinti ambao wako nje ya shule na ndani ya shule
lakini hawa ni ambao wako nje ya shule na lengo letu ni kufikia wasichana wote
na kuboresha suala la soka” alisema shabani.
Kambibi Kamugisha
kutoka shirika la jukwaa la utu wa mtoto CDF alisema kuwa kwa sasa wameanza na
kata Tano ikiwemo kata ya Nyamwaga , Susuni, Sirari, Sabasaba na Matongo na
lengo ni kuelimisha jamii ikiwa ni pamoja na kumpa nafasi mtoto wa kike kattika
kufabnya maamuzi sahihi.
Kwa upande
wake katibu wa chama cha mpira wilayani Tarime Mkoani Mara Sirelia Malai
amesema kuwa kupitia mashindano hayo tayari wamepata timu Nne za wanawakea na
kufikia Agasti Mwaka huu timu hizo
zitakaimishwa kwa baadhi ya Timu ili ziweze kulelewa kwa lengo la kuendelezwa.
Pia
mashindano hayo yameweza kushirikisha wanaume ambapo Timu ya Nyamongo FC na
Songambele Fc wameweza kukutana Fainala ambaopo Nyamongo FC Wamelazwa kichapo
cha bao moja kwa Nunge bao ambalo limefungwa na Ben Maranja mnamo dk ya 55
kipindi cha pili
Nyamongo Fc
walisaka kurudisha bao hilo bila ya kuzaa matunda ambapo mnamo dk ya60 Ben
Maranja kutoka Timu ya Songambele Fc alipigwa kadi nyekundu baada ya kufanya
madhambi
Mashindano
hayo yamemalizika huku mhindi wa kwanza kwa upande wa wanawake akijinyakulia
shilingi lakimoja na mshindi wa pili Elfu hamsini pamoja na upande wa wanaume
shilingi laki moja mshindi wa kwanza na mshindi wa pili shilingi Elfu Hamsini
ambao ni Nyamongo FC.
Lengo la
mashindano hayo ilikuwa ni kufikisha ujumbe kwa jamii kupitia michezo ili
kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo Ukeketaji, Ndoa za Utotoni na mimba za utotoni.
|