RC MARA WAKUU WA WILAYA TEKELEZENI AGIZO LA RAIS
PICHA YA MKUU WA MKOA WA MARA CHARLES MLINGWA |
.
Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt.Charles Mlingwa amewataka
wakuu wa wilaya mkoani mara kuhakikisha wanatekeleza maagizo ya rais wa jamhuri
ya muunganoTanzania ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanamaliza suala la watumishi hewa pamoja na ukamilishaji wa
madawati ikiwemo wilaya ya Serengeti, Bunda na Musoma huku akisema kuwa hatua katika suala la zima la utengenezaji wa madawati
katika shule za msingi ni 93% na Sekondari 98%
huku mkuu wa mkoa huyo akiwataka wakuu wa wilaya ya hao kutetea haki za wananchi wanyonge na
kuwasikiliza kero zao na kuzitetua kwa muda muafaka .
Kauli hiyo imetolewa jana na
mkuu wa mkoa wa mara Charles Mlingwa
pindi akiwaapisha wakuu wa wilaya sita wateule mkoani mara katika ofisi
za makao makuu ya mkoa wa Mara mjini
musoma
Aidha mkuu wa mkoa alisema kuwa wakuu wa wilaya
katika kuapishwa kwa wakuu wa mikoa rais aliweza kuwa maagizo mbalimbali hivyi
hawana budi kuyatekeleza ikiwa ni pamoja na kumlaiza suala la madawati japokuwa
muda ulitolewa na rais umepita.
“Tekelezeni yote muliyoambiwa na mkuu wa Nchi na
mimi mkuu wa mkoa sitakubali kufanyakazi na mkuu wa wilaya atakayeshindwa
kutekeleza majukumu yake sikilizeni wanachi wanyonge na kumaliza shida zao
suala la watumishi hewa hebu tumia kamati za ulinzi na usalama” alisem,a Mkuu
wa Mkoa.
Aidha mkuu wa
mkoa huyo amehimiza wakuu wa wilaya
kuwasimamia wakurugenzi katika halmashauri zao hasa katika suala la fedha za
serikali kutotumiwa hovyo huku wakibuni vyanza vya mapato kwa ajili ya
kuongezea halmashauri hizo mapato na kutumia vyema fedha huku wasimamizi wakuu
wakiwa ni wa kuu wa wilaya katika halmashauri huska.
Wakizungumza na kwa nyakati tofauti wakuu wa wilaya hao baada ya kuapishwa muda mfupi akiwemo
Grolious Luoga mkuu wa wilaya ya Tarime pamoja na mkuu wa wilaya ya Serengeti
na Butiama wameeleza jitihada walizonazo kuhakikisha wanatekeleza maagizo ya
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ikiwa ni pamoja na suala watumishi hewa
, usimamizi wa fedha za serikali , utengenezaji wa madawati.
Luoga alisema kuwa anaenda kutekeleza mara
moja mikakati yote aliyoweka ikiwa ni pamoja na kutokomeza vitendo vya ukatili
wa kijinsia ukiwemo ukeketaji katika wilaya ya Tarime ambayo imeonekana kuwa
kitovu cha ukatili huku akihaidi kuyatekleza maagizo yote ya mkuu wa mkoa pamoja
na Rais.
Zoezi hilo la kuapisha wakuu wa wilaya hao Wateule wameapishwa wakuu wa wilaya sita wilaya sita ambazo ni wilaya ya serengeti ya
bwana Nurdin Babu, wilaya ya Tarime Glorius
Luoga, wilaya ya Rorya Simon Chacha ,wilaya ya Bunda Lydia Simeon ,
wilaya ya musoma Dkt. Vicent Anney , na wilaya ya Butiama Anarose Nyamubi .