DC ATEKETEZA MASHAMBA YA BHANGI.
Kulingana na
zao halamu la kilimo cha Bhangi ambalo limeshamili wilayani Tarime mkoani Mara
mkuu wa wilaya hiyo Glorious Luoga amezidi kuvalila njuga zao hilo kwa
kuteketeza mashamba ya bhangi ili wananchi waweze kuondokana na kilimo cha zao
hilo ambapo katika kitongoji cha Nyahongo Kijiji cha Nyarwana kata ya Kibasuka
yameteketezwa mashamba zaidi ya heka tatu huku zikikamatwa bhangi Magunia 23
yenye uzito wa kilo 769 na gramu93 ambayo ilikuwa imeisha andaliwa kwa ajili ya
kupelekwa ili kuuzwa.
Akiteketeza
mashamba hayo kwa kusirikiana na jeshi la polisi mkuu wa wilaya amesema kuwa
ameamua kufanya msako mkali ili kuweza kutokomeza zao hilo halamu na badala
yake wananci wajikite katika kulima zao halali na kujipatia kipato.
“Unavyoona
mashamba haya yote ya bhangi tutayafyeka yote japo kwa leo hatutamaliza lakini
itabidi jeshi la polisi warudi kwa mara ya pili na kufanya masako mkali ili
kuweza kufyeka bhangi katika maeneo yote yanayolima zao hili halamu mpaka
kilimo hiki kiweze kuisha Tarime” alisema Luoga.
Aidha Luoga
alisema kuwa suala la utumiaji wa madawa ya kulevya ikiwemo bhangi inayolimwa
kinaweza kuwa chanzo kikubwa katika kuchochea uvunjifu wa amani suala ambalo
hatakubaliana nalo na kuhakikisha maeneo yote yanayolima zao hilo halamu
yanamaliza kiliomo hicho.
Bakarani Urio kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmasauri ya
Tarime amezidi kuwasii wanachi badala ya kulima bhangi wajikite katika kilimo
cha Ufuta mahindi pamoja na Mihogo.
Leo tumefika katika mashamba na wanachi wangu mimi kama
kiongozi nawasihi sana waeeze kujikita katika kilimo halali na sisi kama
Halmashauri tutweza kuwaletea pembejeo kwa ajili ya kilimo ili waweze kivuna na
ukiangalia bonde hili ni zuri maji yapo lakini linatumika vibaya alisema
Bakari.