CDF WAZINDUA MRADI WAZEE WA MILA TOENI ELIMU KWA JAMII ILI KUTOKEMEZA UKEKETAJI TARIME.
KATIBU TAWALA WILAYA YA TARIME MKOANI MARA AKIZINDUA RASMI MRADI HUO WA Kukusanya Nguvu za pamoja kulinda na kutetea haki za wasichana katika Mkoa wa Mara na Mwanza. |
Kulingana na vitendo vya ukatili wa
kijinsia na mimba za utotoni vinavyoendelea kutendeka hapa Nchini ukiwemo Mkoa
wa Mara hususani wilayani Tarime, wazee wa mila wameombwa kuingilia kati
na kutoa Elimu wanayoipata kupitia mashirika mbalimba likiwemo shirika la
Jukwaa la utu wa mtoto( CDF) juu ya kupinga vitendo vya ukatili wa
kijinsia pamoja na ukeketajia na ndoa za utotoni ikiwa ni pamoja na umhimu wa urithi wa mali kwa wanawake kwa lengo la
kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidhi na wanawake na watoto wa kike.
Hayo yamebainishwa na katibu Tawala
wa wilaya ya Tarime John Marwa kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious
Luoga katika uzinduzi wa mradi wa Kukusanya
Nguvu za pamoja kulinda na kutetea haki za wasichana katika Mkoa wa Mara na
Mwanza katika ukumbi wa Blue Sky Mjini Tarime mkoani Mara.
Aidha katibu Tawala amesema kuwa
katika jamii ya kikurya kupitia koo zote 13 za kikurya wazee wa mila wanasauti kubwa hivyo hawana
budi kufikisha Elimu juu ya Madhara ya ukeketaji, vipigo kwa wanawake pamoja na
ndoa za utotoni ili kutokomeza vitendo hivyo.
“Wazee wangu nawaomba elimu
mnayoipta hapa na ambayo mmekuwa mkipewa hebu ifikishe kwa jamii ili kuondokana
na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kutambua elimu kwa mtoto
wa kike hala elimu hii itolewa kuanzia mashuleni” alisema Katibu Tawala.
Hata hivyo katibu tawala alisema
kuwa endapo wazee hao wa mila watajitokeza kwa pamoja na kusema hapana katika suala zima la ukeketaji kupitia koo
zote kumi na tau ukatilai utaisha na
kila jamii itaweza kuishi kwa haki bila ya kutendewa unyama wowote huku akizidi
kusisitiza suala zima la Elimu kwa watoto wa kike na kiume nakusema kila mtoto
ana haki sawa hivyo wazazi waondokane na ubaguzi katika familia na kuondokana
na dhana potofu zilizopitwa na wakati.
Sinda Nyangole ni mwenyekiti wa wazee wa mila kutoka wa koo13 za kikurya Wilayani Tarime Mkoani
Mara alisema kuwa nao kwa sasa wamejipanga kwa lengo la kutoa elimu hiyo juu ya
kupinga vitendo vya ukatili wa kijnsia huku akiomba mashirika kuendelea kutoa
elimu hususani maeneo ya vijijini ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo maalumu kwa
waandishi wa habari ili kuandika habari sahihi juu ya kuemilisha jamii madhara
ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ukeketaji na mimba za utotoni.
Akizungumzia lengo la Mradi huo
Mkuu wa Program kutoka CDF Cynthia Mushi kwa niaba ya mkurugrnzi wa
shirika hilo Koshuma Mtengeti alisema kuwa mradi huo umelenga wasichana
wanaoishi katika mazingira hatarishi kutoka mkoa wa Mwanza na Mara ili
kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika jamii ili kuweza kujiendeleza Mwanza
na Mara.
Hata hivyo Cynthia alisema kuwa mradi
huo umezinduliwa rasmi na shirika la jukwaa la utu wa mtoto kwa kushirikiana na
shirika la Forward lililopo UK chini ya ufadhili wa mashirika ya COMIC RELIE na ,SIGRID RAUSING ambapo mradi
huo unatarajia kufanya kazi kwa kushirikiana pia na mashirika ya UMATI lililopo
Musoma, Kituo cha Wadada Centre kilichopo Mwanza ili kuhakikisha msichana
anajengewa uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali juu ya maisha yao ya
kila siku huku wakiwawezesha pia wasichana walioko katika mazingira hatarishi
ili kuzijua haki zao za msingi ikiwemo Elimu.
Katika mkoa wa Mara Mradi huo
umelenga wilaya ya Tarime, Butiama kwa upande wa Tarime mradi huo umelenga kata
za Manga , Matongo, Susuni,Mwema na Nkende huku wilya ya Butiama kata za
Nyegina, Etaro,Kukirango, Nyakanga, na Nyamimanga na kwa upande wa mkoa wa
mwanza mradi huo umelenga wilaya ya
ilemela kata za Kitangiri na Pasiansi.
Hata hivyo Cynthia alisema kuwa
baadhi ya wilaya ikiwemo wilaya ya Tarime wameisha anza kutekeleza mradi hawamu
ya kwanza ambapo mradi huu unatarajiwa kutekelezwa kipindi cha miaka maitatu.
Nao Baadhi ya viongozi wa dini akiwemo
Sheikh mkuu wa wilaya ya Tarime Abdul hakimu Murisho Sud wamezidi kalaani
vikali vitendo vya ukatilia wa kijinsia ukiwemo ukeketaji kwa mtoto wa kike
katika wilaya ya Tarime mkoani Mara na badala yake jamii imkeketa kielimu kwani
wasichan wanafursa nzuri wanapopewa elimu.
Kwa upande wa wasichana ambao
wamekuwa wahanga wa matukio hayo ya Levina Samwel kutoka wilaya ya Rorya,
Rorya Girls Network pamoja na Loveness Enock kutoka Pasiansi Club from Wadada
Centre iliyopo Mwanza wamesema kuwa jamii haina budi kuendelea kmuthamini mtoto
wa kike huku wakiondokana na dhana potofu kuwa mtoto wa kike ni wa kuolewa
badala ya kupewa elimu huku wakiwataka wasichana kujiamini na kujitambua kwa
kusema hapana.